ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 11, 2014

"PENZI LAKO" BY MUSA [Coming Soon Audio] #PenziLako

Kijana mdogo aitwae Musa Shamu (mwanafunzi wa sekondari kidato cha tatu) mwenye kipaji cha pekee cha kuimba anatarajia kuachia rasimi nyimbo yake mpya iitwayo "PENZI LAKO" ina hadhi zinazostahili kwa masikio ya msikilizaji. Producer aliyefanya ngoma hiyo anaitwa BK (BK Mavinanda) chini ya studio ya KAPSTONE ya mkoani Tabora

NI KWELI kuwa vijana wengi wawapo mashuleni huwa na vipaji vingi vikiwemo vya kuimba lakini huishia kutangatanga na wasipopata misimamo mizuri ya vipaji vyao basi hufa moja kwa moja.

Kijana huyu hadi kufikia kuimba na kurekodi nyimbo yenye viwango vyake ni jitihada zilizofanywa na mwalimu wake anayemfundisha katika shule hiyo. Mwl  huyo pia ni msanii anayefahamika kwa jina la Deevon aliyeguswa na kiwango cha kijana huyo na kuhakikisha anamsimamia hadi anafanikisha kuitoa kazi hii ya PENZI LAKO.

Utaipata hapa hapa.

1 comment: