Advertisements

Tuesday, July 29, 2014

SHEREHE ZA EID MKOANI SINGIDA

Sheikh wa mkoa wa Singida na Meya Mstahiki wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Sheikh Salum Mahami, akitoa mawaidha yake kwenye kilele cha Siku kuu ya Eid El-Fitr kilichofanyika kwenye uwanja wa Namfua leo. Pamoja na mambo mengine, Sheikh Mahami amekisihi kikundi cha Ukawa kurudi Bungeni, ili waweze kuwapatia Watanzania Katiba itakayokidhi mahitaji ya zaidi ya miaka 50 ijayo.
Imamu wa msikiti wa Utemini, Jumanne Maghasi, akisoma dua kwenye kilele cha maadhimisho ya siku kuu ya Eid El-Fitr kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu mkoa wa Singida, walioshiriki dua ya Eid-El-Fitr iliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Picha kwa hisani ya Mo Blog

No comments: