ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 2, 2014

UKIONA HII UNAWEZA KUJIKUMBUSHA ULIKO TOKA NA HAPO ULIPO SASA

Hii ni kwa wale tuliokulia mazingira ya ujamaa na kujitegemea tulianza kujitegemea toka umri huu. Je unakumbuka nini ukiona picha hii na hapo ulipo sasa?. Jitiririshe na mawazo yangu hapa chini labda utayapenda au na kuchangia na wewe mawazo yako. Comment nairusha hewani mimi mwenyewe kama utaandika jina lako. 
Wanadiaspora tunaweza kubadirisha kule tuliko toka kwakufanya kitu chochote ambacho tunaweza kujivunia na kuwa kwetu Diaspora. Kwa kidogo tulichonacho twaweza kuleta furaha kwa kizazi cha eneo husika. Tusiwalaumu viongozi, Wakulaumiwa ni wananchi wa eneo husika kwa kuwapa dhamana viongozi walafi wanajali matumbo yao na familia zao tu. Serikali kwa kutokuwa na mtaala maalumu pia sera mbovu walizoziweka.

1 comment:

Anonymous said...

Ramla Ali:
Mimi nilianza kusaidia kazi za nyumbani baadae kidogo kwa sababu nilikuwa na madada wakubwa zangu. Nilibeba maji kuanzia niko darasa la kwanza. Kubeba ndoo kichwani kama mara saba hivi kila siku.(ndoo ya lita kama kumi hivi). Asubuhi kabla ya shule ni kufanya usafi nyumbani. Shuleni pia kuna kuwagilia maua na kufagia uwanja. Kazi za nyumbani kwangu zilikuwa afadhali kiasi kwani tulikuwa wengi tukisaidiana. Ila za shule ndio zilinishinda. Hasa za juani kuokota takataka saa saba mchana na jua kalii. We acha tu. Mwanangu nikimwambia asafishe chumba chake na vacuum cleaner analalamika. Mungu tubariki