ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 15, 2014

Yanga,Twite apewa namba mpya


Nahodha wake wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa,afundishe kikosi cha vijana wa timu 

Katika hatua nyingine, kiraka Mbuyu Twite ameibuka na kumuomba Maximo ampange katika nafasi kiungo aliyokuwa anacheza Athuman Idd na Frank Domayo.
YANGA wanaficha, lakini habari za uhakika ni kwamba Mbrazil Marcio Maximo, amempigia chapuo nahodha wake wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa, afundishe kikosi cha vijana wa timu hiyo.
Maximo anaamini Nsajigwa ataifanyia Yanga kazi nzuri akiwa kocha wa vijana kwa ajili ya kuzalisha vipaji vitakavyotumiwa kwenye timu kubwa.
“Maximo amependekeza Nsajigwa afundishe timu ya vijana ya Yanga na Salvatory Edward aendelee naye kwenye kikosi cha wakubwa pamoja na Mbrazil Leonado Neiva, anataka hivyo kulingana na namna anavyomjua Nsajigwa tangu alipokuwa anamfundisha Stars. Anajua ataisaidia Yanga kama atapewa nafasi,” kilisema chanzo chetu.
Katika hatua nyingine, kiraka Mbuyu Twite ameibuka na kumuomba Maximo ampange katika nafasi kiungo aliyokuwa anacheza Athuman Idd na Frank Domayo.
Wachezaji hao sasa wote hawapo kikosini kwani Domayo amesajiliwa Azam na Chuji ameachwa.
Twite ameonekana katika mazoezi ya Yanga kama anayeandaliwa kucheza nafasi hiyo licha ya uwepo wa Hamis Thabit, Hassan Dilunga ambao wanaweza kucheza nafasi hiyo licha ya kuwa na uzoefu mdogo.
“Hakuna tatizo kama kocha akinipanga namba sita, nitacheza na nakuhakikishia haitanisumbua nafasi hiyo kwani nimewahi kuicheza katika timu zangu za nyuma, hivyo hakitakuwa kitu kipya,” alisema Twite.
“Kabla ya kuja Yanga nilikuwa namudu kucheza namba sita lakini hapa sijawahi kutumiwa katika nafasi hiyo ukitoa hii ninayocheza ya namba mbili na beki ya kati.”
Katika mazoezi ya jana Jumatatu Twite alitumika kuanzisha mipira ya ushambuliaji akiwa na kiungo Omega Seme.By Doris Maliyaga Mwanaspoti

No comments: