ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 1, 2014

YULE MWANAFUNZI WA CHUO ALIYECHOMWA MOTA AFARIKI

Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) enzi za uhai wake.
Muonekano wa marehemu, Daniel Lema baada ya wananchi kumshambulia.
Jeneza la mwili wa marehemu Daniel Lema.
Ndugu wa marehemu wakipamba jeneza la marehemu.Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira akidhaniwa kuwa mwizi.

Tukio hilo lilitokea Juni 24, 2014,majira ya saa 5 usikuambapo inadaiwa kuwa Daniel alikuwa ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia, akawa anatafuta chakula cha jioni ambapo alipofika kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa umefungwa, aliingia ndani ambapo binti aliyekuwa amelala ndani ya mgahawa huo, alianza kupiga kelele za mwizi zilizowakusanya wananchi wenye hasira kali.


Wananchi hao walianza kumshambulia Daniel wakiongozwa na mlinzi mmoja wa jamii ya Kimasai, baada ya kuzidiwa na kichapo wananchi hao walimmwagia mafuta ya taa na kumchoma moto kisha wote wakatoweka. Mwanafunzi huyo aliokolewa na madereva bodaboda ambao walizima moto na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa lakini siku kadhaa baadaye alifariki dunia.

Mwili wa marehemu umeagwa mapema leo katika hospitali hiyo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumatano.

Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA!

2 comments:

Anonymous said...

Wanachi wa Tanzania tubadilikeni jamani hata kama tunahasira kiasi gani please tusichukue sheria mikononi. Najua wizi au kuibiwa kunauma sana but hebu tujaribu kutafuta njia mbadali badala ya kuwachoma moto hawa watu ambapo mda mwingine tunakosea tunawachoma mpaka wasiohusika. Hii habari ya Daniel Lema inasikitisha sana, we fikiria ndio ungekuwa mzazi mmoja wa Daniel ungejisiaje? Lazima tukubali tumefanya kosa hapa tumempoteza Daniel tena alikuwa katika masoma ya kupigania haki. He could have been a good lawyer who can be used by all tanzanians.

REAST IN PEACE BROTHER!!

Anonymous said...

Wote walioshiriki kusababisha kifo cha Lema damu yake inalia juu Yao.Wataiepukaje laana hiyo.?Tujifunze kuepuka laana hizi kwa kisingizio kuwa ni wananchi wenye hasira.Hiyo haikubaliki.Tunasababisha laana hata kwa vizazi vyetu visivyo na laana.Tubadilike.