Mhe. Rais Jakaya Kikwete
Ndugu
Mheshimiwa Raisi, ni kwa moyo mzito na uliojawa na matumaini nachukua nafasi
hii kukujumuisha katika uhalisia wa nchi yetu inapokwenda, ilipo kwa sasa na
ilivyokuwa hapo awali kutonana na mtazamo wangu binafsi. Najua ni wazi kuwa
kila mwenye mapenzi na nchi hii, ukiwemo wewe Mheshimiwa Raisi, unatambua wazi
kuwa nchi yetu ilipo na inapoelekea si kama tulivyotarajia . Katika barua hii,
nitazungumzia kwa ufupi nchi yetu ilivyokuwa hapo awali, ilipo sasa na
inapoelekea pamoja na kutoa mapendekezo jinsi ya kutatua baadhi ya matatizo
yanayotukabili.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, kama
Conficius,mwanafalsafa mashuhuri alivyosema, "Jifunze yakale kama unataka
kuchambua yajayo" nami nitaanza barua yangu hii kwa kuchambua kwa kifupi
jinsi nchi yetu ilivyokuwa hapo awali. Kwa wale wote ambao walijifunza historia
kidogo ya nchi yetu,
tunajua kabla ya mkoloni nchi yetu ilikuwa ikitawaliwa na
tawala za kichifu ambazo zilisisitiza wanajamii wake kuishi kwa kupendana na
ushirikiano. Falsafa ya jamii hizo zenye tawala za kichifu zilisisitiza umuhimu
wa jamii kabla ya umuhimu wa mtu binafsi. Falsafa hii ilijikita katika mila
zetu na kwa asilimia kubwa ilitoa muongozo kwa tamaduni mbalimbali ambao zilichanua
katika jamii hizo. Katika jamii hizo, udini baina ya jamii na jamii ulitawala
na kwa yoyote asiyesoma kitabu cha Kinjekitile anaweza kutambua hili. Hata
hivyo, kutokana na udogo wa jamii hizi pamoja na karibia kila jamii kuwa na
Miungu yake, udini haukuwa tatizo kubwa zama hizo. Baada ya uhuru, jamii nyingi
zilijikuta zikilazimika kubadili mifumo yao ya kitawala na kwa mara ya kwanza
kutii utawala mmoja ambao uliongozwa na Mwalimu Nyerere. Pamoja na uchanga wa
umoja ambao makabilia na watu wenye itikadi mbalimbali walilazimika kuutumika
baada ya uhuru, Watanzania walionyesha mshikamano mkubwa na uvumilivu ambao
uliifanya nchi yetu isifike nje na ndani kutonaka mshikamano huo baina ya
makabila zaidi ya 120 yenye mila na imani tofauti. Kwa ujumla kwa yoyote
atayeangalia jamii hizi za hapo awali,
atatambua kuwa jamii hizi ziliungana kutona na kuwa na adui mmoja ambaye
alikuwa mkoloni na mshikamano na heshima baina ya jamii hizi uliendelea baada
ya uhuru kutokana na uhalisia kuwa jamii zao zilipitia unyasasaji na unyonyaji
uliofanana kutoka kwa mkoloni. Neno uzalendo nyakati hizo lilikuwa na maana
kubwa na uongozi uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere haukusita kuwawajibisha
wale wote ambao walikuwa hawana uzalendo katika kuliongoza taifa letu. Kama wote
tunavyojua, sera za Mwalimu Nyerere zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika
kuleta umoja baina ya Watanzania hata hivyo zilishindwa kukabiliana na
changamoto za kiuchumi zilizoikumba jamii yetu. Hata hivyo, pamoja na sera za
kimaendeleo za Mwalimu Nyerere ambaye alifuata sera za Kijamaa zenye sura ya
Kiafrika kushindwa katika sekta ya uchumi, Mwalimu alitambua umuhimu wa elimu
kwa katika maendeleo yetu na alifanya kila awezalo kuhakikisha unongozi wake
unatilia mkazo elimu. Kofi Annan, moja ya nyota za Afrika zilizongara katika
jukwaa la kimataifa aliwahi kusema," elimu ni haki ya binadamu na ina
nguvu kubwa ya kumbadilisha. Katika misingi yake, mihimili ya uhuru,
demokrasia na maendeleo endelevu
hupatikana." Mwalimu Nyerere kwa kulitambua hili, hakusita kutilia mkazo
wa kipekee katika elimu hata pale alipotambua wazi kuwa sera zake za Kijamaa
hazikuwa zikizaa matunda yalitarajiwa.
Baada ya Mwalimu kuachia madaraka na
Mzee Mwinyi kuchuka nchi, Tanzani ilijikuta katika ya dunia ambayo ilikuwa
ikipitia mabadiliko makubwa kama mwisho wa Ukomunisti katika Jamuhuri ya
Kisovieti na Demokrasi kuchua uongozi kama mfumo katika serikali nyingi
duniani. Mnamo mwaka 1992, kama wote tunavyofahamu, Tanzania haikuwa na budi
ila kuingiza mfumo wa vyama vingi nchini kama njia mmojawapo ya kukuza
demokrasia. Hata hivyo, mfumo wa demokrasia haukukosa kasoro katika jamii
ambayo ilikuwa imeunganishwa na sera za ujamaa. Demokrasia pamoja na ukosefu wa elimu ulikuwa ukiwakumba
Watanzania wengi kwa nyakati hizo, ulisababisha mabadiliko makubwa ya jamii
yetu ambayo kwa mara ya kwanza iliruhusu watu wenye itikadi tofauti za kisiasa
na kidini kujadili tofauti zao hadharani. Bila kutazamia, jamii yetu ilianza
kuwa na matabaka ambayo yaliletwa na utofauti wa kipato, maarifa pamoja na itikadi
za kisiasa lakini tafaouti hizi zilikuwa za kutarajia kwa jamii yoyote ile
ambayo ilikuwa katika mabadiliko makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Baada ya miaka karibia 21 ya mfumo
wa nyama vyingi na miaka 51 na moja ya kujitawala, jamii yetu imepitia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, siasa na
kijamii. Sera kama za Ujamaa zimebaki kuwa sera zinavyofundishwa mashuleni bila
kuwa na nguvu katika uhalisia. Vile vile, demokrasia ambayo ilikuja na chembe
za ubepari(soko
huru), imefanya jamii yetu ya sasa kuwa na tofaouti kubwa kati ya matajiri na
maskini. Mbali na hayo, mabadiliko ya kidunia ambapo vita dhidi ya ugaidi
vimepewa vipaumbele katika sera za mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi,
zimefanya nchi yetu ijikute katika changamoto zisizozuhilika kutokana na muundo
na upeo wa jamii yetu.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, sote
tunatambua kuwa katika kila badiliko ambalo jamii yoyote ile itapitia, lazima
kuwe na changamoto mbalimbali ambazo zitajitokeza. Kwa wale ambao walibahatika
kusoma historia ya dunia kwa ujumla, watatambua kuwa mabadiliko ya kiuchumu,
kisiasa na kijamii ambayo yalitokea
katika nchi mbalimbali hapo karne za awali,yalitawaliwa na machafuko makubwa.
Bila kupoteza dira ya mjadala huu, nchi yetu kwa sasa inakumbana na changamoto
za kiuchumi, kidini, kisiasa na kijamii kutokana na mabadiko mbalimbali ambayo
nchi yetu imepitia na inayoendelea kupitia.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, changamoto
za kiuchumi nchini kwetu zinaletwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia na baadhi ya
sera zisizo na tija ambazo serikali yetu zinatekeleza. Ndugu Mheshimiwa Raisi,
nadhani bila shaka unatambua jinsi serikali yako inavyoshutumiwa kwa kutokuwa
makini katika sekta ya uchumi. Kila kukicha wabunge wetu wanatuonyesha
Watanzania jinsi serikali yetu isivyo makini katika kusimamia miradi ya
kiuchumu pamoja na upotevu wa mamilioni ya shilingi unaoletwa na uzembe huo.
Mikataba mibovu, viongozi wasio na upeo pamoja na uzembe wa usimamizi wa miradi
ni baadha tu matatizo ambayo yanakuza tatizo la uchumu dhoofu katika nchi yetu.
Mheshimwa Raisi, nadhani wimbo huu si mgeni katika masikio yako na bila shaka
unafanya kila uwezalo kama unavyotakikana na katiba na sera ya chama chako
kutafutia ufumbuzi tatizo hili la uchumi. Hata hivyo, Mheshimiwa Raisi kwa
kiasi kikubwa sera za chama chako zinaruhusu tatizo la uchumu kuendelea kukua
na mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wakiendesha nchi kwa kutumia uzoefu bila
tija na utalaamu unaohitajika hivyo kufanya tatizo la uchumu kukua kila
kukicha.Mheshimiwa Raisi, katika nakala hii nataka kukujulisha vile vile jinsi
jamii yetu unavyochangia katika tatizo la uchumi.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, baada ya sera ya Ujamaa
kushindwa kuzaa matunda katika sekta ya uchumi, na nchi yetu kukumbatia
demokrasia na ubepari(soko huru), asimilia kubwa ya jamii yetu haikuwa tayari
kielimu kakabiliana na mabadiliko haya. Mheshimiwa Raisi, kama wote
tunavyotambua, ili demokrasia iweze kufanikiwa, lazima kila mwananchi afahamu
majukumu yake katika maendeleo ya kiuchumi na awe na utashi wa kuyatekeleza
majukumu hayo. Sio siri kutokana na mfumo wa vyama vingi na ushindani unaoletwa
na mfumo huu, baadhi ya vyama zimeelekeza juhudi zao kuwashawishi Watanzania
kuwa jukumu la kuleta maendeleo kwa asilimia kubwa ni la serikali kwa kutoa
ahadi zisizo za kweli. Utegemezi huu kwa serikali umezalisha jamii ambayo kwa
kiasi kikubwa haiwajibiki katika kujiletea maendeleo. Mheshimiwa Raisi,
natambua wazi kuwa Serikali yoyote ile iko madarakani kutoa muongozo stahiki
kwa wanachi wake ili kuwaletea maendeleo katika sekta mbalimbali. Hata hivyo,
kwa mataifa ambayo yameendelea, wananchi wake huwajibika kwa asilimia kubwa
katika kujiletea maendeleo na kazi za serikali zao hubakia kuwa ni kutengeneza
mazingira yanayostahili ili wananchi wake waweze kutekeleza mipango yao. Katika
nchi yetu kumekuwa na matatizo mawili makuu katika suala hili. Kwanza kabisa
asilimia kubwa ya wananchi wamelazimishwa kuamini kuwa jukumu la kuleta
maendeleo kwa asilimia kubwa, ni la serikali, na vile vile serikali yetu
imekuwa haitengenezi mazingira stahiki kwa wananchi wake kutekeleza mipango yao
hivyo kuwavunja moyo wale wachache wenye kutekeleza majukumu yao. Uzembe huu wa
serikali unatokana na siasa zenye chembechembe za ushabiki wa sera za kijamaa.
Kwa mfano, nchini mwetu ni jambo la kawaida kusikia wizara fulani au sekta
fulani inatawaliwa na watu wa kabila au itikadi fulani.Tatizo hili la upendeleo
ambalo husababisha utendaji hafifu kutonana na watendaji wa sekta hizo
kutowajibishana ipasavyo, misingi yake iko katika elimu haba ambayo Watanzania
wengi wanaendelea kuipata, na waliyopata, wakati wanabadili mifumo ya kisiasa
na kijamii miaka ya tisini. Jamii yetu haikuelimishwa vizuri njia mbadala za
kuachana na sera za kijamaa, na mwishowe tumejikuta tukiandamwa na ujamaa
katika zama ambazo tumeipa demokrasia nafasi kubwa katika mfumo wetu wa
kuendesha nchi. .
Ndugu Mheshimiwa Raisi, changamoto
nyingine ambayo inaikabili jamii yetu kwa sasa ni ile ya udini. Changamoto hii
kwa asilimia kubwa imezaliwa na muelekeo wa sera za mataifa yenye nguvu
kiuchumu duniani na nchi yetu imekumbwa katikati ya tatizo hili. Kama sote
tunavyojua, suala la ugaidi ni suala tete ambao watu wengi hulitafsiri isivyo
na kusababisha uhasama baina ya watu wa madhehebu mbalimbali. Ugaidi
kuambatanishwa kimakosa na dini yenye wafuasi wengi duniani, kumesababisha
kutokea kwa uhasama baina ya Waislamu na watu wa madhehebu mengine. Waislamu
wanaamini wameonewa kwa dini yao kufananishwa na Ugaidi na hivyo basi kuchukua
jukumu la kuilinda dini yao. Mheshimiwa Raisi, sitazungumzia kwa undani jinsi
dhana hii potofu kuwa Ugaidi unaletwa na Waislamu wenye kufuata miiko ya dini
yao, bali nitaongelea kwa ufupi jinsi uhalisia wa hali hii unavyojitokeza
katika jamii yetu na kutoa mapendekezo jinsi ya kupambana nao.
Mheshimwa Raisi, siamini kuwa mtu au jamii yoyote ile ina haki ya
kunyooshea vidole dini nyingine kwa sababu tu kuna baadhi ya wafuasi wa dini
hiyo wanahusishwa na matukio ya fulani. Hata hivyo,kwa upande mmoja ni jukumu
la viongozi wa kidini kutoa tafsiri stahiki za maandiko ya kidini ili kuepusha kutoposhwa kwa ukweli wa
maandiko hayo. Pamoja na misingi ya tatizo hili la udini kutokea nje ya nchi
yetu,baadhi ya wanasiasa wetu wamekuwa wakitumia suala hili la udini kupenyeza
sera zao kwa wananchi.Viongozi hawa ni wazi wanatakiwa wawajibishwe ipasavyo
kwani kiongozi yoyote yule katika jamii ana ushawishi mkubwa kwa watu, hivyo
basi lazima katiba itimike ipasavyo kuelezea mipaka ya ushawishi huu walionao
viongozi wetu. Serikali haina budi kushughulikia kwa urahaka na bila upendeleo
tofauti zote za kidini ambao zinazojitokeza ndani ya nchi yetu pamoja na kutoa
elimu itakayowaelimisha wananchi namna mbadala ya kuishi kwenye jamii iliyo
chini ya serikali isiyo na dini.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, hivi
karibuni tumeshudia kwa huzuni kubwa asimilia sitini ya watahiniwa wa kidato
cha nne wakifeli katika mitiyani yao hivi juzi juzi. Mheshimiwa Raisi, yote niliyozungumzia hapo awali
hatayakuwa na umuhimu wowote kama watu ambao taifa letu linawategemea kuleta maendeleo ya kifikira, kisiasa, kijamii pamoja na kiuchumi hawana ufamu wa
kina wa mambo. Hali hii ya sasa nchini inakatisha matumaini ya maendelea yoyote
yale kwani ili kutela maendeleo, lazima wananchi wale na maarifa toshelezi
yanayoendana na nyakati ambayo yatawawezesha kupanga na kutekeleza mipango sanifu
ya kimaendeleo. Vile vile, lazima wananchi wawe na uelewa wa kutambua nafasi
yao na ya serikali katika kujiletea maendeleo. Mheshimiwa Raisi, pamoja na
kutambua kuwa serikali yetu ina changamoto nyingine ambazo zinahitaji
kushughulikwa kwa haraka kama ukosefu wa maji, umeme na miundombinu, sekta ya
elimu ni uhai wa taifa lolote lile na sote tunafahamu hili. Mheshimiwa Raisi,
nchi yetu iko katika dunia ambayo inapiga hatua kubwa katika sekta ya elimu
ambayo manufaa yake yanaonekana kwenye kila ngazi katika jamii mbalimbali
duniani hivyo basi hatuna budi kuacha mzaha na sekta hii.
Ndugu Mheshimiwa Raisi, mwisho wa
barua hii napenda kuwapongeza na
kuwakosoa wanasiasa wetu ambao wamekuwa wakijituma kuwaletea Watanzania
maendeleo na vile vile kwa nyakati nyingine wamekuwa wakileta matatizo katika
harakati zao za kisiasa. Mheshimiwa Raisi, sio siri kuwa kwa sasa nchi yetu
imekumbatia Demokrasia kwa mapana yake na kwa asilimia kubwa wanasiasa wetu
wameanzisha utamaduni wa kuwajibishana wao kwa wao kwa nia ya kumletea
maendeleo Mtanzania wa kawaida. Wanasiasa wanaonyesha ukomavu na uvumilivu
mkubwa unaotakikana katika demokrasia bila kuleta machafuko ya kisiasa ambayo
yamekuwa yakiwakumbwa majirani zetu. Hata hivyo, katika zama hizi ambazo
demokrasiia inashamiri, wanasiasa wengi wamekuwa wakitumia vibaya Watanzania
kueneza siasa za chuki na kidini wakisisitiza wanapiginia demokrasia.Mheshimiwa
Raisi, natambua kwa mapana ya haki kujielezea kama inavyoelezwa na misingi
demokrasia, lakini pamoja na mapungufu ya serikali yetu, baadhi wanasiasa
wamekuwa wakiweka ushabiki wa kisiasa mbele katika kukosoa au kupongeza
serikali yetu. Vile vile, serikali yako imekuwa haitoi ushirikiano stahiki kwa
wanasiasa wa baadhi wa vyama vya upinzani hivyo basi kuwafanya watumie njia
ambazo mara nyingine husababisha machafuko katika jamii wakati wa kuwakilisha
kero za wananchi wao. Mheshimiwa Raisi, ili kuendelea kuienzi amani yetu,
serikali yetu inapaswa kushirikiana na wadau wote katika siasa bila upendeleo
unaotokana na itikadi za kisiasa au kidini ile kumletea Mtanzania wa kawaida
maendeleo ya kweli. Wanasiasa nao lazima watumie njia mbadala kuwakilisha kero
za wananchi na kufichua uzembe wowote ule kwa upande wa serikali na wananchi
bila uchochezi huku wakiendelea kuwajibishana wao kwa wao.
Mheshimiwa Raisi, najua kwa asilimia
kubwa yote niliyoyazungumza kwenye barua hii si masuala mageni masikioni mwako, na ninatumaini utaendelea
kuchukua hatua stahiki kwa ushikiano na wananchi, viongozi wa kisiasa, kidini
na taasisi mbalimbali katika kulikumbusha taifa misingi yake ambayo
inahatarishwa na mabaliko ya kidunia,kijamii, kidini na kisiasa nchini kwetu .
Mungu
ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.
Dennis John,
Mtanzania
Mkereketwa.
Well written. I
ReplyDeleteDennis man what a joke! Umeandika garbage nyingi. Wewe ni ukawa au Chadema puppet?We are doing well as a country! Of course we have more work ahead of us, lakini Tanzania inasonga mbele. Maybe not at the speed of your liking mr. Fake Dennis! Assuming that we elect you as the next President, please post on this blog your five years development plan. Unfortunately, the use of cheap pseudo-names such as Dennis and the likes, would only advance the interest of the opposition at the expense of Tanzanians. Mimi ni mtanzania ambaye nimechoshwa na watu wanao mdharau Rais ambaye alichaguliwa na mamilioni ya watanzania. People like Dennis should just shut up, and I mean it!
ReplyDeleteNdugu "Anonymous", ni wazi ufahamu wako kwenye masuala fulani muhimu ni haba. Sidhani kama umesoma vyema barua hii kwa jinsi ulivyocomment. Muhandishi wa barua hii amepitia kwa umakini vipengele ulivyozungumzia na vile vile ameonyesha mawazo komavu kwa kutambua kuwa na pamoja kuwa tuko nyuma kimaendeleo tumepiga hatua kubwa kimaendeleo toka tulipopata uhuru. Vile vile, hamna kipengeleo chochote katika barua hii ambacho kinamkashifu Raisi Kikwete kama unavyodhani na pia muhandishi wa barua hii amekemea kwa asilimia kubwa jinsi wapinzani wanavyotumia jukwaa la vyama vingi kukwamisha maendeleo. Kama msomaji wa barua hii nimesikitishwa na jibu lako ambalo linanifanya nitilie shaka umri na uwezo wako wa kufikiri, yaanii kwa upeo wako wewe umeona ushabiki wa chama au kejeli kwa Raisi Kikwete katika barua hii na kwa wakati huo huo unajiita Mtanzania aliyechoshwa na ushabiki wa chama?
ReplyDeleteHello! My name is Dennis and I claim the responsibility for the content of this letter. Dear "anonymous",following your comment I was lost of appropriate words to address your stance! However, it was obviously you didn't read the letter as your comments projected.I clearly highlighted how we have great strides in development and how relative comparison of our development to other developed country can be totally unfair give majority of the developed countries took a couple of centuries to advance! "Ukawa"?, Chadema? I had to go back to my letter and try to find where I seemed to advance the agendas of the mentioned groups without success, kindly point out the specifics and I'll gladly respond. If you had read the letter, you might concluded that to a greater extent I was critical of the opposition while at the same time acknowledging their efforts in challenging for a better Tanzania. Secondly, I personally hold Hon. Kikwete in high esteem(I'll vote for him if it were possible for him to run again by the way!) that's why I invited him to share my thoughts of how we can build a better foundation for any sustainable development.My letter didn't suggest I was critical of any development plan laid forward by Hon. Kikwete, but I urged him to spearhead the culture of accountability, enforce quality education, eradicate religious barrier and fairness in order to pave a smooth path for your apparent "five plans".I am not sure if further explanation is worth my time since your mediocre response to my article does not suggest you are willing to reason critically although I'll like to believe otherwise.
ReplyDelete