Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Estelina Sanga ‘Linah’ na Nasib Abdul ‘Diamond’ wakicheza kwa pamoja katika uzinduzi wa Serengeti Fiesta 2014 jijini Mwanza.
Wakati wawili hao wakiteka hisia za mashabiki kutokana na jinsi walivyokamua huku wakicheza shoo, pia wasanii mbalimbali nao walifanya vitu vyao jukwaani hapo, wachanga kwa wakongwe wakiwemo Young Killer na Mo music waliokuwa wenyeji.Wakizidi kuwarusha mashabiki wao.
Wengine waliopata fursa ya kufanya makamuzi ya nguvu ni pamoja na Yamoto Bendi, Sky Light, Makomandoo, Chege na Temba, Madee, Nay wa Mitego, Stamina, Young Dee, Mr Blue, Nyandu Toz, Khadija Maumivu, Vanesa Mdee na baadaye Dogo Janja aliyepanda jukwaani ikiwa ni siku chache baada ya kutimiza umri wa miaka 18.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake