Albert Ebosse.
Shirikisho hilo liliamua kusimamisha mechi zote hadi pale mikakati mipya itatangazwa itakayodhibiti utovu wa nidhamu na kuhakikisha usalama wa wachezaji.
Shirikisho hilo limeahidi kutoa ruzuku ya dola laki moja kwa jamaa na familia za Ebosse kiasi sawa na mshahara wake iwapo angemaliza kandarasi yake katika klabu hiyo ya JS Kabylie .
Isitoshe kila mchezaji wa klabu hiyo atatoa mshahara wake wa mwezi mmoja kusaidia jamaa yake Ebosse.
Awali Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou alionya kuwa Afrika haitatumika kama chimbuko la utovu wa nidhamu.
Bwana hayatouy aliyasema hayo baada ya mshambulizi wa JS Kabylie kutoka Cameroon Albert Ebosse kupurwa na jiwe kichwani akafa katika ligi ya Algeria.
Hayatou aliagiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa ilikukabiliana na utovu wa Usalama.
Ebosee mwenye umri wa miaka 24, aligongwa kichwani baada ya timu yake kushindwa mabao 2-1 na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Mamlaka nchini humo imeagiza kufungwa wa uwanja wa 1st Novemba 1954 .
Ebosse alikuwa mfungaji bora msimu uliokamilika akiwa na jumla ya mabao 17 tangu awasili nchini humo kutoka Malaysia.
Rais wa ligi kuu ya Algeria Mahfoud Kerbadj, alisema kuwa kifo chake ni msiba mkubwa kwa soka ya nchi hiyo.
BBC
No comments:
Post a Comment