Advertisements

Thursday, August 21, 2014

KUTOKUBALI MATOKEO YA UCHAGUZI WA JUMUIYA DMV 2014

 
Ismail Mwilima aliyekua mgombea wa Katibu

TUME YA UCHAGUZI WA JUMUIYA DMV USA/WANAOHUSIKA.

Nataka kuchukua nafasi hii kwa kusimama kwa masikitiko makubwa, na manung'uniko mengi toka kwenye moyo wangu. Kwani vitu na vitendo mbalimbali vili tokea na kufanywa na watu mbali mbali ndani ya kituo/vituo vya uchaguzi mnamo tarehe ya 09/08/2014. Mimi siku hiyo ya uchaguzi (09/08/2014) sikuwepo hapa DC Metro Area kwa sababu zisizo zuilika . Ila nilikuwa miongoni mwa wana jumuiya walio kuwa wakigombea nafasi ya Ukatibu wa jumuiya yetu ya DMV. Ila nimesikia na kuelezwa kwa kirefu kuwa vitendo vingi ambavyo havikuwa vya kihalali,haki na kikatiba vilitendeka katika uchaguzi huu ulio pita. Kwa sababu hiyo mimi Ismail Mwilima nakataa na sikubali matokeo ya uchaguzi ulio fanyika tarehe 09/08/2014.

Sababu zinazo nifanya nisikubali matokeo haya ni hizi zifuatazo:

1. Tume ili kutana na sisi wagombea pamoja na balozi Liberatus Mulamula na ika kubali kufanya mambo yafuatavyo.
(a) Wagombea wasio weza kuwepo siku ya 09/08/2014 watapewa nafasi ya kujieleza kupitia mtandao/video katika siku ya uchaguziili wapiga kura waweze kusikia sera za mgombea. ( Tume uchaguzi tarehe 09/08/2014 haiku onyesha video yangu ambayo niliwatumia waonyeshe kwa wana jumuiya ndani ya siku ya uchaguzi kama tulivyo kubaliana katika ofisi ya balozi).

(b) Tulikubaliana Kura zote zipigwe muhuri nyuma kuhakikisha uharali wake.(nasikia kura hazikupigwa muhuri nyuma).

(c) Absentee ballot ( Nasikia tume ya uchaguzi haiku angalia, kusoma na kuhesabu kura za wana jumuiya walio nje ya kituo/vituo ya kupigia kura).

(d) Nasikia baadhi familia/ndugu ya walio kuwa mgombea/wagombea kataka nafasi tofauti katika uchaguzi huu ulio fanyika 09/08/2014.

Walionekana wakigawa karatasi za kupigia kura kwa watu tofauti. (Hawa wanafamilia hawakutakiwa wagawe karatasi za kupigia kura).

(e) Nasikia kuwa kulikuwa na baadhi ya wapigaji kura ambao walipiga kura zaidi ya mara moja. (siku zote hairuhusiwi mtu yeyote yule apige kura zaidi ya mara moja).

(f) Nasikia kuna kura zilizo zidi hazikuwa ndani ya majina ya watu walio jiandikisha katika zoezi hili la kupiga kura. (kwa hiyo nataka nijue hizi kura zilizo zidi zilitokea wapi).

(g)Nasikia mmoja wa wana jumuiya alizichukua kura zote zilizo pigwa na kuzipeleka anapo jua yeye, kabla ya zoezi la kuhesabu kura halija malizika kitendo ambacho sija kielewa mpaka sasa.

(h) Mwisho nasikia taratibu za kikatiba hazikufuatwa kama katiba inavyo sema kuhusu taratibu za kabla ya upigaji kura, wakati wa kupiga kura na baada ya kupiga kura.

KWA SABABU HIZI NA NYINGI MOYONI MIMI ISMAIL MWILIMA SIKUBALI NA SIHALALISHI MATOKEO YA UCHAGUZI ULIO FANYIKA 09/08/2014.

NDUGU WANA JUMUIYA ASANTENI SANA KURA ZENU, UPENDO WENU, USHIRIKIANO WENU, MICHANGO YENU, MAOMBI NA DUA ZENU NA MAMBO MENGI AMBAYO MLINIPATIA KATIKA KIPINDI HIKI MUHIMU CHA KUTAFUTA VIONGOZI BORA WA JUMUIYA YETU TUMAYO IPENDA KIDHATI. HAKIKA WANA JUMUIYA WA DMV MPO KWENYE SEHEMU YA KIPEKEE NDANI YA MOYO WANGU NA DAIMA HAMTA SAHAULIKA AU KUFUTIKA NDANI YA MAISHA YANGU. NA NINAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUWALETA NYIE NDANI YA MAISHA YANGU HAPA DMV. ASANTENI SANA BWANA ALIYE MBINGUNI AWABARIKI WOTE DAIMA.

NDUGU NA KIPENZI CHENU DAIMA.

ISMAIL MWILIMA
21/08/2014

14 comments:

Anonymous said...

Kama wewe unataka kuwa kiongozi,unaandika habari ya kuwa "nimesikia","nimeambiwa",sasa kweli ukiongoza na habari za kuambiwa,si utatupeleka shimoni??kura ulizoshindwa ni nyingi,hauhitaji kuwa super genius or rocket scientist kujua kuwa u lost. USHAURI,Jiunge na Kamati zilizopo kwani tunahitaji mchango wako. Onyesha busara kama wewe ukiwa Mwenyekiti wa Vijana CCM,maana una experience tosha za uchaguzi

Anonymous said...

hhahahahah waaaaaaooo, hear saying!!!! what is this dj. why are you posting such article. is amazing about hear saying. well get a lawyer like other dawg

Anonymous said...

Jamani poleni sana. Mimi nina suluhisho na malalamiko yenu. Wote mlioshindwa mmekataa matokeo. Sasa anzisheni jumuiya yenu maana mmesema mna wafuasi 223 na muite Watanganyika-DMV. Viongozi wenu wawe kama ifuatavyo

1.Rais- Liberatus
2.Makamu Rais- Salma
3.Katibu- Ismail
4.Makamu katibu- Solomon
5.Mweka Hazina- Mmoja wa wafuasi wenu.

Tayari mna timu, si mnataka kuwa viongozi hiyo hapo tayari jumuiya ya wanachama 223 ambao hata hamhitaji kulipia uanachama kama hii ya watanzania--DMV.

Kila la heri watanganyika wenzangu,na mimi nitakuwa mwanachama mkereketwa kabisaaa.

Anonymous said...

uliyetoa comment hii wewe una akili timanu au, nadhani wewendo utawaka yule starring uliyenganania kile pahali pamoja na watoto ,na wajuku na virembwe wako wote kwenye uchaguli na kuzibana bana kura ili ashinde iddy.

tumia busara umeshakuwa mtu mzima hapo ulipo si teenager tena.

kwani tanzanania/Tanganyika zipo mbili? kama hazipo mbili basi jumuiya lazima iwe mmoja.
na kama mmeiba kura za watu na kufanya huu uchaguzi uwe wa vituko na kichekesho ni lazima watu watasema mtake mistake.

Anonymous said...

Anonymous wa 2:3 PM -you said it best. That is exactly I was thinking, why not form another Jumuiya, you all have 223 members, already, start with the new Katiba, no need of michango, man your Jumuiya will only grow everyday, because every Tanzanian in DMV will be in you Jumuiya -si hakuna michango right? And one more question, what happened to all those michango ya kuchukua lawyers -what is the update on that???

Anonymous said...

Mmmh yaani huyu jamaa kaamua kukaa kabisa chini na kufungua kompyuta yake ili aandika 'aliyoambia kuwa yalijiri siku ya uchaguzi' aise kweli ni vizuri hukushinda manake ungeweza kukigawa chama kwa mambo unayosikia kwenye radio mbao. Dah umetisha!

Anonymous said...

Heeee heeee?!! WHAT A TEAM!! DJ LUKE atakuwa halali mirejesho from Rais na video from Makamu!! Kaaaaa kweli eti waanzishe nyingine... WATU gani wasiokubali kushindwa.

Anonymous said...

TUNAAMBIWA WEWE NI KBARAKA UNATUMIWA JE NI KWELI? HATA HAYO MAELEZO YANAJIELEZA TUAMINI HIVYO?

Anonymous said...

niliju tu utabana comment lakini za kumponda jamaa umeziweka,what a shame dj luke

Anonymous said...

Mfyuuuu kihelehele kinakuwasha mludishe pesa zetu za uanachama mlizobeba na tutaanzisha chama chetu bas

Anonymous said...

Hahahaaaa hilo nalo nenooo! !! Anzisheni jumuiya yenuu au kama mnaweza hameni kabisaaa nendeni mkaishi kwinginee marekani kubwaa hii, lol..wakosa haya nyie rohoo mbayaa tuu!!! IDDY NDO CHAGUO LETUU MTAKE MSITAKE NA UCHAGUZII HAURUDIWIII! !! JIPANGENI UPYAA!!!

Anonymous said...

Wewe mwandishi huna busar hata kidogo.ignorant

Anonymous said...

Ignorant

Anonymous said...

dj luke mtendeeni na yeye haki muhojini kama mlivyo wahoji wanina salma moshi na libe kwenye clip tumsikiye.
ahsante