Migogoro mingi ya kimapenzi ni makosa ya watu kupita mlango wa Shetani.
Tukiendelea na mada yetu; Mapenzi siku zote yanaweza kuwa asali kama wahusika wataamini katika nguvu ya maneno. Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na mapenzi husuluhisha migogoro ya muda mfupi.
Wapenzi wanaponuniana, endapo watakutana faragha, hasira zote hupotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, utamu wa maneno mazuri ni zaidi ya kutosheka kimwili. Kwa maana hiyo wapenzi hawana budi kuzungumza kwa maelewano ili kuufanya uhusiano wao kuwa asali siku zote.
Kwa mfano, ndoa nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo chanzo cha kila kitu.
Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna kitu kigeni.
Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote. Ukishazoeana na mwenzi wako hasa baada ya kuwa pamoja muda mrefu, utaanza kujiachia. Ni kipindi ambacho mmoja anaweza kuhisi amesalitiwa kwa sababu mwanzoni hakuona hivyo ‘vitabia vya kuudhi’, alifichwa.
MAPENZI NI KARATA TATU
Kuna msemo kuwa mapenzi hayashindwi ila watu ndiyo hushindwa na mapenzi. Tunarukia kwenye uhusiano bila kuwa na uhakika ni kiasi gani tunawapenda wenzetu na ni kwa kiwango kipi tumejiandaa kubeba majukumu.
Mwisho wa siku tunafeli. Tatizo ni kwamba tunaanzisha uhusiano mpya bila kutatua kasoro zilizosababisha tukashindwa kwenye uhusiano na mtu wa kwanza. Hapo nadhani unaweza kuona kwamba wakati mwingine mapenzi siyo tata ila wenyewe tunayafanya kuwa magumu.Tuna mambo mengi, ya kifamilia, kikazi, imani, dini, kabila, tofauti za kimtazamo na matarajio ya kila mmoja.
GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake