ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 13, 2014

MAGUFULI AKAGUA MIZANI YA KISASA

 Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Ndugu Kileo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli jinsi Mzani mpya wa Vigwaza utakavokuwa ukipima magari wakati yakitembea tofauti na mizani mingine nchini.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya ujenzi  inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo katika eneo la Mloganzila Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Dkt. Magufuli alipita hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Wakanadarasi wakati wa ziara yake yakutembelea na kukagua ujenzi wa   barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments: