Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Ndugu Kileo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli jinsi Mzani mpya wa Vigwaza utakavokuwa ukipima magari wakati yakitembea tofauti na mizani mingine nchini.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya ujenzi inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo katika eneo la Mloganzila Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Dkt. Magufuli alipita hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Wakanadarasi wakati wa ziara yake yakutembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake