Monday, August 11, 2014

Mchanganuo wa report ya Tume

MCHANGANUO ZAIDI KUTHIBITISHA UCHAKACHUAJI WA UCHAGUZI WA August 9, 2014

MCHANGANUO HUU UNAENDELEA KUTHIBITISHA KUWA UCHAGUZI WA AUGUST 9, 2014 NI BATILI


Tumesoma mchanganuo wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mzee Safari na ametoa mahesabu ambayo yanazidi kuongeza sintofahamu. Huu ni mchanganuo wa kutengenezwa ili kuwapumbaza wana DMV; “Team Libe for DMV President 2014”  itathibitish ubatilii huu pasi na shaka.  Tunanukuu mchanganuo huo wa Tume hapa chini. Kama ifuatavyo;

Mchanganuo wa Tume ya Uchaguzi kutoka kwenye report ya mwisho.
Yafuatayo ni matokeo ya ukaguzi  wa mfumo wa kura uliobainisha hitilafu:
a)Idadi ya wapiga kura walioko kwenye orodha ya wanachama  hai:   586. Wanachama 150 waliamua kutopiga kura.
b) Wanachama waliopiga kura kituoni: 436
c) Kura za ghaibu ( in absence): 14 Mgawo wake ni:  Libe 9 na Iddi 5
d) Kura zilizo toka kwenye masanduku na kuhesabiwa na mawakala: 445:  Katika hizo mawakala wa Libe waliripoti kura 214, na wa Iddi waliripoti kura 231:  Kwa hivyo kuna kura za ziada  kwenye masanduku kuliko idadi ya wapiga kura.  Ziada hiyo ni kura 9.

           Kutokana na mchanganuo huu wa kupikwa, naomba msomaji shirikiana na “Team Libe for DMV Community 2014” ili tuthibitishe udanganyifu wa Tume ya Uchaguzi na Board of Trustee chini ya Hamza Mwamoyo.
            Mzee Safari anasema; Wanachama hai ni 586, wanachama ambao hawakupiga kura ni 150; na waliopiga kura kituoni ni 436.  Mzee Safari anaongeza kuwa; waliopiga kura za ghaibu (absentee ballot) ni 14.
            Sasa basi, shirikiana nasi kufanya mahesabu ya darasa la kwanza kwa kujumlisha waliopiga kura kituon 436, ambao hawakupiga kura 150 na waliopiga kura za ghaibu (absent) 14; (436+150+14= 600).  Rejea hapo juu orodha ya wanachama hai ni 586, lakni jumla inaonyesha 600: KWA NINI NUMBER STILL DON'T ADD UP!

Endelea...
http://libe4dmvpresident2014.blogspot.com/2014/08/mchanganuo-zaidi-kuthibitisha.html

1 comment:

  1. Mambo mliyafanya kuwa makubwa as if mnachagua raisi wa nchi..acheni mbwembwe,.mambo makubwa wakati bajeti yenu bado yamanati..tulizeni mwembwe. Libe rudi zako kazini, hayo uliosema wakati wa kampeni unaweza yatimiza hata bila kuwa kiongozi wa wana DMV. Hapo DC kuna ukirutimba mkubwa sana..mko wengi. .mmesoma vizuri tuu but bado uswahili mwingi..dah!..very sad but somehow funny!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake