Advertisements

Thursday, August 21, 2014

MCHUNGAJI MBATTA ASEMA ALISHIRIKI MKUTANO KWA SIMU LAKINI HAKUTIA SAINI TAMKO LA WACHUNGAJI HEBU JITIRIRKIE MWENYEWE

Mchungaji John Mbatta.

Wachungaji wametoa TAMKO lao kufuatana na walivyoona zoezi zima la uchaguzi lilivyotekelezwa. Sioni katika TAMKO hilo kama kulikuwa na kosa kwa wagombea u-Raisi na wala sioni kama kuna u-Dini katika TAMKO hilo. Bila kufumbia macho, inaonekana kama kuna kasoro kadhaa wa kadha zilizojitokeza katika utekelezaji wa uchaguzi kwa ujumla.

Kwanza kabisa sikuwako kwenye mkutano wa wachungaji physically. Sahihi ya kalamu inayoonekana kwenye TAMKO siyo ya kwangu. Mimi  nilitoa maoni yangu kwa wachungaji kwa njia ya simu. Na  kutokana na nilivyosoma katika mitandao mbalimbali iliyokuwa ikiandika  habari za uchaguzi. nilibaini kwamba kulikuwa na kasoro kadha wa kadha katika utaratibu mzima wa kupiga kura. Kasoro nilizo zisoma kutoka mitandao ni kama:
  1. Inasemekana kampeni ziliendlea wakati wanajumuiya wana piga kura. Kama ilikuwa hivyo, hilo haikuwa sahihi.
  2. Baadhi ya wapiga kura inasemekana hawakuwa na vitambulisho vya jumuiya, ambazo hasa ndizo zingetumika kupiga kura (Au stakabadhi ya malipo ya uana-jumuiya).
  3. Inasemekana kura zilipohesabiwa kulikuwa na kura za ziada ambazo haikujulikana zilitoka wapi, na hii ilimfanya hata mwenyekiti wa uchaguzi kupata kigugumizi kutangaza majibu ya uchaguzi na alikaririwa akitamka “This election is void”.

Mambo kama haya yanapotokea siyo ya kupuuzwa. Nivema kutafuta njia ya haraka kufikia suluhisho na kuondoa kasoro hizo. Huwezi ukaanza kugawa kura zilizozidi kama suluhisho, hiyo ni kuzidisha kasoro.

Nilipendekeza kuwa, ofisi ya Balozi ambayo ni mdhamini wa Jumuiya iwaite Wagombea u-Raisi, Wachungaji na ma-Sheikh, wakae pamoja kuzungumza kwa heshima, busara na hekima ili kupata maridhiano na suluhisho litakalozuia mpasuko unaotaka kujitokeza. 

14 comments:

Anonymous said...

Tunashukuru sana mtumishi wa Mungu kwa kujitokeza kuzungumzia kasoro za uchaguzi. Lakini mtumishi bado hujamtaja mchungaji mwenzenu aliyegushi sahihi za wachungaji wenzie. Hilo nalo ni tatizo ambalo bado linatia kiwingu mawazo yako mazuri na ya busara. Kabla ya kufikia hatua uliyoipendekeza, tunaomba kila mchungaji aliyetajwa kwenye barua ya malalamiko ajitokeze na kutoa msimamo wake ikiwa ni pamoja na kukubali au kukanusha kama alitia sahihi barua yenu. Pia tunawaomba kwa pamoja mkubali kumtaja mchungaji aliyegushi sahihi zenu. Kama hilo halitofanyika namuomba mh. Balozi atupilie mbali barua yenu iliyo gushiwa sahihi kwa kuwa siyo halali.

Anonymous said...

Mchungaji naomba uelewe kuwa masheikh na mapadri wakatoliki hawahusiki na madai yenu.

Anonymous said...

Msipomtaja aliyegushi sahihi ubalozi hauwezi kusikiliza suala lenu. Wakatoliki na waislamu hawahusiki kabisa na mdai yenu. Muwaache. Wachungaji DMV mmejishushia heshima. Wote mlikuwa kanisa moja, iweje mkagawanyika??????

Anonymous said...

Tatizo hapa ni sahihi zenu zilizogushiwa. Tunashukuru kwa kujitokeza na tunaomba uwashauri wenzako waliobaki waige mfano wako. Tunaomba mtuambie nani kati yenu aliyegushi saini zenu?????? Msimsumbue mh balozi.

Anonymous said...

Barua yenu ilikuwa inatoa tamko la wachungaji. Iweje leo unawashirikisha masheikh?

Anonymous said...

Mchungaji unasema ulishiriki mkutano kupitia conference call na hukuwepo mkutanoni physically, je, uliruhusu mchungaji yeyote aweke sahihi kwa niaba yako????? Je, masheikh walishiriki conference call na kuandika majina/sahihi kwenye barua yenu? Unajuaje kama wao wanashiriki malalamiko yenu?

Anonymous said...

Unakiri kuwa sahihi ya kalamu inayoonekana siyo ya kwako, tunaomba utuambie ni ya nani?? Na kwanini huyu mtu atumie jina lako bila idhini yako?? Barua yenye tamko la wachungaji ni halali?? Kama barua siyo halali, kwanini balozi awaite??

Anonymous said...

Duh aisee mungu awashinde yaani mnawasingizia uongo mpaka wachungaji!! Mkiulizwa?uchaguzi

Anonymous said...

Kama hamkuwashirikisha masheikh na mapadri kwenye conference call na barua yenu iliyosainiwa na mtu asiyejulikana, kwanini uwaombe masheikh washiriki mkutano ubalozini?

Anonymous said...

Nina maswali kwa wana DMV
1. Je mna sheria au katiba ya kuongoza chaguzi zenu? Hizi sheria zenu au kanuni zinasemaje? Mmekwenda kwa wataalamu wa mambo ya sheria akawashauri what is the best course of action? Nimemsikiliza Libe, Solomon na Dada Salma, wote wanasema kanuni za uchaguzi zilivunjwa au kukiukwa, ni zipi hizo? hebu wekeni wazi your guiding principles as DMV ili wenye upeo wa sheria wawasaidie.
2.Kwenda mahakamani - hili ni gharama sana, litachukua muda wenu na nguvu zenu, na kama hamna sheria zenu za umoja - mtachalenji uchaguzi based on what?
3. Uchaguzi ni gharama, wanajumuiya wamesafiri wameacha mambo yao ili kupiga kura je mmewauliza wale wote walio piga kura kama wanataka uchaguzi urudiwe? Nani atalipa gharama zao kuacha mambo yao kuja kupiga kura tena? unless you have electronic voting system in place.
4. Ushauri wangu (kama independent neutral Tanzanian) mwenye mapenzi mema na umoja wenu, ambaye sina interest na nani ashinde au ashindwe, Kaeni pamoja muone jinsi ya kushirikisha mawazo mazuri kutoka kwa viongozi na walio nje ya uongozi. I heard you all said DMV first, yes this the time, wandugu, one thing unites you, Tanzania. Do you want to fight in courts for this? you know how long a court process will take? how much money?Your time and energy? How will this cost the Umoja you want to serve? There will be an injuction or something to stop activities of the Umoja until the determination of the suit righ? Seriously you want to go on record as the Tanzanins who sued each other because of leadership of a Umoja? I hate injustice in any form or shape, however, ask yourselves what do you want to achieve? Anyway, all the best and make sure you have enough money to sustain litigation in the US. Nice weekend all!

Anonymous said...

Nimeelewa vizuri maoni ya Mchungaji Mbata. Ameeleza kwa hekima na kupendekeza kuwashirikisha viongozi wengine ili kwa pamoja muone jinsi ya kushirikisha mawazo mazuri kutoka kwa viongozi hao ku solve differences zilizojitokeza katika uchaguzi wenu. Kulazimisha watu waseme nani alitia sahihi, ina maana hamna nia ya kumaliza mkaraba wenu.

Anonymous said...

Ndg wachangia hoja na wanaDMV wote, balozi si mwamuzi wa mwisho wa jambo hili. Mwamuzi wa mwisho ni sheria ya nchi hii. Hapa siyo Tanzania tulikozoea kudhulumu haki za watu kwa kutumia vyeo, udini,ukabila,kujuana,rushwa nk. Balozi ni mpatanishi wa familia tu hii DMV na akishindwa kutoa haki USA justice inachukua mkondo wake. Nawashukuru wachungaji, wadau wa haki na team Libe kwa pamoja na wapiga kura wao wote, watu mbali mbali wanaounga mkono haki na uhuru katka chaguzi za kidemokrasia duniani....... kwamba nyie wote mmetibua uozo na uvundo uliojificha aidhha miaka mingi ndani ya uongozi huu mdogo shina/chimbuko likiwa toka nyumbani Tz. Tamko la wachungaji lisippoungwa mkono hata mawe yataliunga mkono, tamko lao halimlazimishi balozi kuchukua hatua. Sheria nayo isipofanya hivyo kihatua, Mungu atafanya mwenyewe ili kukomesha dhuluma.

Anonymous said...

Siku zote "Success" ni mjukuu wa kila mtu na "Failure" ni mtoto yatima!!! Usemi huu unataka kujidhihirisha katika swala la tamko la wachungaji. No pastor should defect if he took part in putting together the press relase, regardless of whether or not it has been well-received. Hakuna sababu ya kuwa vuguvugu kama mwanasiasa. Mchungaji Mbatta, stand fully behind it; there's nothing wrong with the press release.

Anonymous said...

WEWE ANONYMOUS WA #12, SHERIA GANI UNYOZUNGUMZIA. HAMNA BASE YA CASE, RUSHWA GANI UNAYOSEMA. HUYU MGOMBEA WAKO YEYE MWENYEWE ALISEMA ANAYO IMANI NA TUME KABLA YA UCHAGUZI. SASA KWA NINI HAKUJITOA KAMA ALIKUWA HANA IMANI. WALK TALK AND TALK WALK. #GET A LIFE