Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kwanza wa Diaspora katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Agosti 14, 2014 Picha na Ikulu
Ndugu zangu,
Leo alfajiri niliongoza mjadala kwenye redio za Kwanza Jamii na Nuru FM kuhusiana na kongamano linaloendelea Dar la Watanzania wa Diaspora wanaokutana nyumbani, Tanzania.
Ni kwa nini tuna hofu na Watanzania wenzetu walio ughaibuni? Hofu hii ni ya kihistoria.
Kwanini kongamano hili la kwanza kufanyika lisiwe la mwisho kufanyika katika sura yake hii, kwamba maudhui ya kongamano yenyewe kuwa ni ; connect, engage, inform and ivest nako kunakosekana dhana integration kwa maana ya kujumuisha.
Hoja kubwa kwa sasa ni kwa namna gani tunawajumuisha wenzetu walio ughaibuni kupitia uraia pacha. Kwamba wakati umefika wa kubadilika na kuona kuwa uraia pacha una maanufaa makubwa kwetu kama taifa. Haipaswi kuendelea kuwachukulia wenzetu walio diaspora kama ' Ng'ombe wa Maziwa'- Fuatilia mjadala huu...
http://www.mjengwablog.com/hab
1 comment:
Asante. angalau ng'ombe wa maziwa anapewa majani. Mimi naona tunafanywa mabuzi tu. akiumwa mtu unabipiwa utoe chochote, akifaulu kijana wa kaka ndio hivyo tena, akioa mdogo wako uchunike, akiolewa binamu hivyo hivyo. Ukirudi nyumbani uombe pa kufikia wanakusema kukaa kote ulaya mbona hata pahale hana.Hata mwanao ambaye umri wa kupiga boksi hajafikishwa anaombwa pesa, viatu. Ndugu, jirani na marafiki. Ukifikwa na tatizo haooo wanakukacha. Na serikali pia inataka ituchune.
Post a Comment