Kamishna Kova akiwa na RPC mpya wa Temeke, Kihenya Kihenya.
Kamishna Suleiman Kova akionesha namna mguu huo wa mtu mwenye ulemavu unavyotumika kutunzia dawa za kulevya.KIJANA mmoja ambaye ni mlemavu wa mguu, Said Tindwa (36), mkazi wa Vijibweni Kigamboni jijini Dar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutumia mguu wake wa bandia kwa ajili ya kutunzia na kuuza dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova alisema mlemavu huyo alitiwa nguvuni Agosti 1 mwaka huu kufuatia mtego uliowekwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kuziuza dawa hizo kwa kuzificha kwenye mguu wake wa bandia.
Aidha Kova alisema kuwa dawa alizokuwa akiziuza mlemavu huyo ni zile za viwandani kama vile cocaine, heroin na wakati mwingine bangi.
“Katika mtego maalum uliowekwa na askari wa upelelezi ndipo mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa wateja wake baada ya kuzitoa alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo wa bandia” alisema Kova.
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment