MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI WAUNGUA Msikiti maarufu wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam waungua. Hadi muda wa saa moja na nusu usiku huu, magari ya zima moto yameonekana eneo la tukio yakijaribu kuuzima moto huo, ingawa kazi ya kuuzima imeonekana kuwa ngumu kutokana na moto kuanzia ghorofa ya juu ya msikiti huo. Magari ya zima moto yanaendelea kutafuta mbinu ya kufikisha mipira ya maji juu ya jengo hilo, ambalo chini huwa ni msikiti na juu ni madrasa. Hizi ni baadhi ya picha za tukio kama zilivyotumwa na mwandishi wa Global Publishers aliyeko eneo la tukio.
PICHA: SHAKOOR JONGO/GPL |
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake