ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 26, 2014

MWANAMKE KABLA YA NDOA, ANATAKIWA AWE‘AMETOKA’ NA WANAUME WANGAPI?-2


MPENZI msomaji, wiki iliyopita katika mada hii ya ‘mwanamke kabla ya ndoa anatakiwa awe ‘ametoka’ na wanaume wangapi’ tuliishia kwa kumsikiliza bibi mwenye miaka 76 akisimulia mwanamke anavyotakiwa kuwa kimapenzi kabla ya ndoa.

Alisema: “Ukimuona mwanamke mpaka anaolewa ameshalala na wanaume zaidi ya watano hadi sita huyo ana hulka ya umalaya na hatakuwa mwaminifu katika ndoa. Kama una historia ya mwanamke wa sampuli hiyo jaribu kufuatilia nyendo zake.”
SASA ENDELEA…

Akizungumzia historia yake kimapenzi, bibi huyo alisema aliolewa akiwa na umri wa miaka 17 na mpaka wakati huo alikuwa ameshalala na wanaume wawili tu, akiwemo aliyemuoa. Kwa hiyo bibi huyo alilala na mwanaume mmoja tu kabla ya ndoa.

UKWELI WA UTAFITI
Utafiti wa mwandishi wa makala haya umegundua kuwa wanaume wengi hawapendi kuoa wanawake wenye rekodi ya kutembea na wanaume zaidi ya watano mpaka wanapoingia kwenye ndoa na yeye kuwa wa sita.

KUNA WIVU WA HISIA
Wako wanaume wanaosema kuwa waliyaondoa mapenzi kwa wake zao baada ya kugundua kwamba kabla ya kuwaoa walishatembea na wanaume zaidi ya saba mpaka kumi.

Wanasema bado wivu hujengeka hata kama wanaume hao walitembea nao miaka mingi nyuma, lakini ile hali ya kukumbuka au kujenga picha jinsi mkewe alivyokuwa ‘akiwapanga’ wanaume husumbua kichwa na kupandisha hali ya wivu na kutomwamini tena.

John Lucas mkazi wa Sinza jijini Dar yeye anasema msichana aliyepanga kufunga naye ndoa (alimtaja kwa jina la Anna) alimwacha baada ya siku moja kila mmoja kuweka bayana idadi ya wenza wao waliowahi kuwa nao kimapenzi.

“Mwenzangu aliniambia kuwa alishatembea na mwalimu, wakaachana. Akatembea na dereva wa magari ya serikali, naye pia wakaachana.

Akaja akatembea na mtangazaji mmoja wa redio, lakini wakaachana. Mpaka anakutana na mimi alikuwa ametoka kuwa na uhusiano na jamaa mmoja wa wilayani Kinondoni (Dar). Hapo alikuwa na miaka 21 tu. Nikaona hajatulia, nikachemsha, nikammwagia mbali,” anasimulia John.

HISIA ZA KUTOAMINI

Kikubwa alichokiona John, anasema: “Nilihisi akiwa na mimi kama mumewe bado atakuwa na tamaa za kutoka nje ya ndoa kwani tayari ameshajikomaza kwa kulala na wanaume mbalimbali. Angenisumbua kwa kweli.”

MENGINEYO
Tabia ya mwanamke kutembea na wanaume wengi humfikisha mahali anapewa jina la ‘jamvi la wageni’ au ‘maharage ya Mbeya’.

USHAURI WA BURE!
Ni vizuri kama mwanamke ukiolewa halafu siku moja mumeo akikuuliza idadi ya wanaume uliowahi kufanya nao mapenzi kabla ya ndoa yenu, umwongopee. Hii itakusaidia kulinda ndoa pia kudumisha mapenzi halisi kutoka kwake lakini katika uaminifu wako wote. Siyo uongope halafu bado ukawa ‘moto chini ‘, kwenu utarudi..!

KWA WANAUME NAO
Katika zama hizi, si sahihi wanaume wakachukulia mada hii kama kigezo kwamba wao ndiyo wanatakiwa au wana uhalali wa kutembea na wanawake wengi kabla ya ndoa kwani mapenzi yenye rekodi nzuri yanasaidia pande zote katika uhusiano.

GPL

2 comments:

Anonymous said...

WANAUME WANALIMIT YA KULALA NA WANAWAKE WANGAPI KABLA HAWAJAOA?WENGINE WANAKUJA NA VIRUSI KIBAO

Anonymous said...

Kuna wanaume pia ambao wanakuwa na wapenzi wengi sana kabla ya ndoa.hii mada i apply kwa pande zote pls.na ninaamini kwamba baadhi ya watu wanabadilisha wapenzi kwa sababu hujampata yule unaeona atakufaa.you kiss alot of frogs to meet the prince.na pengine ukimpata unaempenda unatulia kabisa.
Huwezi kusema huyu ni wa tatu sasa lazima niolewe nae ili nisije itwa malaya,hata kama hakufai.