Divas wa Skylight Band kutoka kushoto Aneth Kushaba AK47, Mary Lucos na Digna Mbepera kwa pamoja wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiwanja chao cha nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.
Mary Lucos akifanya yake jukwaani.
Hashim Donode a.k.a Mzee wa Kiduku akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Digna Mbepera pamoja na Sam Mapenzi.
Sam Mapenzi (kulia) sambamba na Sony Masamba (katikati) pamoja na Joniko Flower wakisebeneka Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Mupe Salute...Salute mashabiki wa Skylight Band wakishuhudia burudani ya kikosi cha Band inayojikusanyia mashabiki lukuki kutoka kila kona ya nchi ya Tanzania pamoja na nje pia.
Twende hapa ni burudani tu.
Mdau Maso (kushoto) akiwa na marafiki zake ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita walipojumuika kula bata na Skylight Band.
Babu Athumani na Tophy Bass wa Skylight Band nao walipata ukodak.
Mdau akishow love na mshirika wa wadananda.
Le Manager her self Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band sambamba na Digna Mbepera Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Digna Mbepera na hakubaki nyuma naye alisongesha burudani kama kawaida.
When Jesus Say Yes Nobody Can Say NO...! Le Manager her self Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka kwa raha zao kwa kujinafsi.
Sam Mapenzi akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Mashabiki wa Skylight Band wakipata swagga za kinigeria kutoka kwa Sam Mapenzi (hayupo pichani).
oohhh na na na na...ye ye ye ye ye...oohhh na na na na....ye ye ye ye ye...oohhh na na na na....ye ye ye ye ye...Si mwingine ni Sam Mapenzi akiwadatisha mashabiki wa Skylight Band.
Taratibu kwa raha zao wapenzi wa Skylight Band wakiburudika na burudani kutoka kwa Sam Mapenzi (hayupo pichani).
Umati wa mashabiki wa Skylight Band ukiwa umefurika ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Kwa raha zao wakiburudika na Live Band kutoka Skylight.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band na rafiki yake wakipata raha na burudani ya aina yake kutoka Skylight Band.....Wewe je unasubiri nini?? tujumuike leo jioni pamoja Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
Drums ni kiungo muhimu sana kwenye muziki wa Live Band....Idirisa ndiye aliyekuwa akisababisha upande huo.
Mashabiki wakiendelea kuburudika.
Hapa ni burudani na sisi ndio habari ya mujini...Joniko Flower akiongoza kikosi kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band aliyekua akisheherekea siku yake ya kuzaliwa akiimbiwa wimbo maalum wa kusheherekea siku yake maalum na hii yote ni kuwa karibu baina ya Band na mashabiki wao......Wewe na yule pia mnakaribishwa leo kusheherekea siku yako ya kuzaliwa pamoja na Skylight Band.
Oooh mashabiki wawili waliheseherekea birthday zao ndani ya kiota cha Thai Village huku wakijinafasi kwenye dancing floor walipokuwa wakiimbiwa wimbo maaluma na Skylight Band.
Birthday Girls wakipata Ukodak kutoka kwa mashosti zao.
Diva's wakipata Ukodak backstage wakati wakivuta pumzi kabla kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Emma Bass akipata ukodak na murembo mkareeee.
Kubwa kuliko ni ule wakati wa kuzungusha mduara..mmoja wa mashabiki alimua kumwaga radhi kwa namna ya aina yake huku umati wa mashabiki wa Skylight Band ukiwa umefurika na kuduarika vilivyo.
Wakaka wakionekana kupagawishwa na mauno ya mwanadada huyo mwishowe kwenda kumtunza.
Wake kwa waume wakiduarika na Skylight Band.
Joniko Flower akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake