Advertisements

Wednesday, August 27, 2014

TANZANIA DMV KUSHIRIKI LIGI NDOGO JUMAMOSI AUG 30, 2014 NA NEW YORK KUELEKEA MASSACHUSETTS

Timu ya Tanzania DMV

Timu ya Tanzania DMV Jumamosi itashuka dimbani katika ligi ndogo itakayoshirikisha tim kutoka Angola, Botswana, Soth Africa, Zimbabwe na yenyewe Tanzania yote ni katika kusherehekea Labor Day weekend ambayo ni mwisho wa wiki hii Mechi hizi zitaanza kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Park ya Valley Mills kwenye add ya 1600 E Randolph Rd, Colesville, MD 20904

Timu ya New York

Timu ya New York Jumapili asubuhi itaelekea Massachusetts kwenye mechi na timu ya huko katika kusherekea Labor Day weekend. Timu hiyo siku ya Jumapili Aug 24, 2014 ilifanya mazoezi ya pamoja na kukubaliana kwa kauli moja safari ipo na timu itaanza safari ya kuelekea Boston saa 1 asubuhi.

Uongozi wa timu hiyo umetoa usafiri kwa wachezaji kwenda na kurudi na baadhi ya wachezaji wamesema wao watatangulia huko tangia siku ya Ijumaa.

1 comment:

Anonymous said...

haya nduguzetu hii sio ny jitahidini huko kila la kheri