Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Chadema, John Mnyika
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema Rais Kikwete ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi suala la kulisitisha Bunge Maalum la Katiba na siyo mtu mwingine.
Umoja huo pia umeendelea na msimamo wa kumtaka Rais kuwasiliana na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kulisitisha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Chadema, John Mnyika, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kusema hakuna kifungu kinachomwezesha Rais kulisitisha Bunge hilo.
Sefue alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (siyo Nipashe) kuwa “ Hakuna mpango huo kwa hivi sasa, Bunge Maalum la Katiba limeanzishwa na linaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na sheria hiyo haina kifungu cha rais kulisitisha”
Mnyika alisema rais katika hotuba yake ya Julai mwaka huu alitoa ahadi ya kuingilia kati mazungumzo ya vyama vya siasa nchini endapo yatakwama.
“Hatumtaki mtu yeyote aingilie kati suala hili, tunamtaka rais mwenyewe, hatumtaki Wasira, wala Sefue, wala Sitta,” alisema Mnyika.
Aliongeza kuwa Rais Kikwete ana madaraka ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bunge hilo Maalum la kulisitisha Bunge, na endapo Mwenyekiti huyo akakataa ushauri huo, rais ana mamlaka ya kuzuia matumizi mabovu ya pesa za wananchi zinazoendelea kutafunwa katika Bunge hilo.
Alisema Ikulu wasikwepe wajibu wa rais, kwa kuwa rais anamadaraka makubwa ya kuamua mambo pindi panapotokea migogoro ya kivyama ndani ya nchi.
Alisema Rais aitishe maridhiano baina ya vyama hivyo na endapo yatashindwa, Bunge hilo lisivunjwe bali lifanyiwe marekebisho makubwa ikiwamo kurekebishwa kwa sheria lengo likiwa ni kuokoa matumizi mabaya ya fedha yanayoendelea.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake