Mganga mkuu wa Halmashauri ya Ushetu DR Andrew Emmanuali akisisitiza jambo juu ya Mfuko wa CHF katika baraza la madiwa wa halmashauri hiyo
Katibu Tawala wa mkoa wa shinyanga A.Tarimo mwenye miwani akiwa anasikiliza baraza la madiwa wa halmashauri ya ushetu
Baadhi ya wangeni walikwa wakisikiliza baraza la madiwani.
Mh Diwani wa kata ya Iboja kupitia chama cha maendeleo chadema Akisisitiza jambo kuhusu tume iliyopelekwa kuchunguza tuhuma za kukatisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo .
Mwenye kofia ni mkurungezi wa Halmashauri ya ushetu isabela chilumba akiwa na katibu tawala wa mkoa wa shinyanga Tarimo wakati wa kikao cha baraza la madiwani .
Mganga mkuu wa Halmashauri ya ushetu DR Andrew Emmanuari akijibu hoja toka kwa madiwani wa Halmashauri hiyo juu ya matibabu ya kuhusu CHF kwa umakini zaidi
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya ushetu wakiwa makini kusikiliza moja wa mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi ya Halmashauri hiyo .
Na Mohab Dominick
Kahama,
Agosti 20 ,2014
WANANCHI WATAKIWA KUTAMBUA MFUKO WA CHF
WITO umetolewa kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu wialayani Kahama Mkoani Shinyanga kujiunga na Mfuko wa hifadhi ya jamii (CHF) ili kupunguza gharama zinazowakabili wananchi wakati wa matibabu Hospitalini.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya Ushetu Adrea Emmanuel katika kikao cha kawaida cha balaza la madiwa kilichofanyika mjini Kahama ambapo alisema madiwani wanajukumu la kuwahamasisha wananchi juu ya mfuko huo.
Emmanuel Alisema kuwa lengo la mfuko huo sio kuwaumiza wananchi wa halmashauri ya Ushetu bali ni kuwapunguzia gharamaza matibabu na kumrahisishia mwananchi wakati anapokuwa ameambukizwa marazi pamoja na kumsaidia wakati amelazwa katika holspitali yoyote ndani ya Tanzania.
Aliongeza kuwa ili kuwa mwananchama katika mfuko huo wa (CHF) kila mwananchi anatakiwa kuchangia gharama kiasi cha shilling 3000 hadi 5000 kwa kila mwaka ili kupata huduma iliyobora zaidi.
Alisema suala la usimamizi wa ugawaji wa dawa pamoja na kukagua katika vituo vya afya sehemu mbalimbali ni la (Dmo) pamoja na stafu nzima ya afya ndani ya halmashauri hiyo.
Aidha alisema kuwa kazi ya ofisi ya ushirika katika halmashauri hiyo ni kusimamia suala zima la ugawaji wa dawa pamoja na utoaji wa huduma kwa jamii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Katika hatua nyingine Emmanuel alisema kuwa umoja na mshikamano ndio msingi wa kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa ndani ya Halmashauri hiyo hivyo madiwani wanatakiwa kuwahamasisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara waweze kuutambua mfuko huo wa jamii (CHF )
No comments:
Post a Comment