Advertisements

Wednesday, August 20, 2014

YANGA NA SIMBA WAGAWANA VISIWA

Nembo za timu ya Yanga na Simba 
By Doris Maliyaga na Mwanahiba Richard (email the author) 

Simba imeanza matizi mjini Unguja lakini Yanga imetua Pemba kwa mbwembwe na kutangaza kwamba Alhamisi lazima wapige mechi na silaha zake zote zitakanyaga nyasi kupambana kwa mara ya kwanza.

MASHABIKI wa soka mjini hapa wamepagawa baada ya Simba na Yanga kuvamia na kugawana visiwa kwa staili ya aina yake.
Simba imeanza matizi mjini Unguja lakini Yanga imetua Pemba kwa mbwembwe na kutangaza kwamba Alhamisi lazima wapige mechi na silaha zake zote zitakanyaga nyasi kupambana kwa mara ya kwanza.

Mashabiki wa Dar es Salaam ambao waliishuhudia Yanga ikikwea Pipa kwenda Zenji wakadai hii ni noma sana, hatuwezi kukubali tusiione chama la Yanga mara ya kwanza uwanjani huku na wenzao wa Simba wakidai lazima wavuke maji kuona kwa macho yao. Kocha wa Simba, Patrick Phiri amewaangalia wachezaji wote ndani na nje na akasema: “Mbona wapo freshi tu?”

Phiri wa Simba ambaye programu yake siriazi ya mazoezi ilianza jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Chuoni uliopo nje kidogo ya mji, amesisitiza kwamba anahitaji mazoezi makini ya siku mbili tu kufanya uamuzi wa mwisho wa kubadili au kutobadili kikosi.

Kocha huyo ameliambia Mwanaspoti mjini hapa kwamba hataangalia umaarufu wa jina la mchezaji bali jitihada binafsi. Uongozi umemhakikishia kumpa sapoti ya kila namna.

“Sioni kama timu ina matatizo makubwa, yaliyopo ni ya kiufundi tu, naweza kusema Jumatatu ndio nimeanza kazi rasmi hivyo siku kama mbili hivi nitaona kama kuna haja ya kusajili tena vinginevyo hawa niliowaona ni wazuri nawanafaa kuleta ushindi,’ alisema Mzambia huyo.


“Kikubwa nilichogundua kwa sasa ni kwamba wachezaji wana nidhamu ya mchezo, wanajituma na ninaona wanaelewa kwa haraka kile ninachowafundisha ingawa sijakaa nao kwa muda mrefu, lakini pia mechi za kirafiki zitatusaidiakurekebisha makosa yatakayokuwepo, nimewaambia viongozi wanitafutie mechi nane zikiwamo za kimataifa lakini bado sijaambiwa nitacheza na timu gani.


“Nataka kila mchezaji aelewe vizuri ili Simba ilirudishe hadhi yake, ni jukumu langu kuzungumza na mchezaji mmoja mmoja na kujua tatizo lake ili aweze kufuata kile ninachokita uwanjani.”


YANGA HADHARANI


YANGA imetua Pemba jana Jumatatu kwa usafiri wa ndege maalumu, waliondoka Dar es Salaam katika makundi manne na kufikia kwenye hoteli ya kitalii ya Misali iliyopo eneo la Wesha.


Lakini hiyo siyo ishu. Kali ni kwamba Wanzazibari ndiyo watakaokuwa wa kwanza kuiona Yanga ikicheza mechi uwanjani baada ya mazoezi ya karibu miezi miwili mfululizo Dar es Salaam. Mbrazili Maximo kwa mara ya kwanza ataishusha Yanga uwanjani kucheza mechi ya kirafiki keshokutwa Alhamisi dhidi ya Chipukizi ya Pemba kwenye Uwanja wa Gombani.


Yanga imekuwa akifanya mazoezi tu na haikushiriki Kombe la Kagame linaloendelea Rwanda ambapo nafasi yao ilichukuliwa na Azam FC.


“Pemba ni mahali tulivu, naamini tutafanya maandalizi yetu kimya na kwa ubora,”alisema Maximo ambaye amekwenda na wachezaji 27 na viongozi wa benchi la ufundi wanane ndiyo msafara kamili wa Yanga utakaokaa Pemba kwa siku 10.


Wachezaji ni Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ ambao ni makipa. Mabeki wa pembeni ni Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Edward Charles na Amos Abel na mabeki wa kati ni Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Rajab Zahir na Pato Ngonyani.


Viungo ni Mnyarwanda Mbuyu Twite, Said Makapu, Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit. Mastraika ni Mbrazili Genilson Santos ‘Jaja’, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu wakati mawinga ni Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfan na Mbrazili Andrey Coutinho.
CREDIT:MWANASPOTI

No comments: