ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 16, 2014

YANGA UGHAIBUNI INASISKITIKA KUTANGAZA MSIBA WA MCHEZAJI WAKE MOHAMMED ALI

Timu ya Yanga ughaibuni inasikitika kutangaza msiba wa mchezaji wake aliyefariki siku ya Ijumaa Aug 14, 2014 Clevelnd, Ohio na maziko yanatariwa kufanyika kesho huko huko Cleveland Ohio. 
Aliyesimama wa kwanza kushoto ndiye Mohammed Ali enzi ya uhai wake akiwa katika mechi ya Yanga na Simba iliyochezewa Columbus, Ohia May 28, 2011 na Yanga kufungwa na Simba bao 5-2 Pia marehemu alishawahi kuwa mmiliki wa mgahawa wa Taste of Zanzibar. Uongozi na wachezaji wote wa Yanga ughaibuni unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu, tunakuombeeni kwa mwenyezi Mungu awatie nguvu na aiweke roho ya marehemu pema peponi, Amin.

3 comments:

Anonymous said...

In nah ill ah wainah Lillah rajiun

Anonymous said...

HEEE SIJAIONA VIZURI HII PICHA NA WEWE PIA UMMOOOOOO NY IBRA.EEEH.HAYA HAYA MPWA KADOGO

Anonymous said...

R.I.P. Nakumbuka kumuona Taste of Zanzibar. pia alikuwa anafanya catering kwenye events nyingi sana ... Gone too soon...