ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 8, 2014

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV YA KUSANYA PESA NA VITU KWA KITUO CHA WATOTO SUMBAWANGA


Jumuiya ya Watanzania ya DMV (Washington DC, Virginia VA na Maryland MD) yachangisha hapo hapo $819 dollars kwenye mkutano wa kwanza wa jumuiya na kumkabidhi sister Mariastella Wampembe kwa ajili ya matumizi ya kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Katandala Sumbawanga. Kituo hicho kina  watoto wadogo wapatao 86 ambao baadhi  huokotwa vichakani, chooni na wengine hutelekezwa mbele ya milango ya kituo  wakiwa na umri wa siku moja. Vile vile kituo hicho kina shule ya msingi na Sekondari yenye  wanafunzi wapatao 500.

Jumuiya Pia ilitoa vitabu zaidi ya 600 vya Masomo mbalimbali kwa kituo hicho.

Jumuiya bado inapenda kuwajulisha kuwa bado tunaendelea kukusanya vitu mbali mbali kwa ajili ya kituo hicho:

Vitu Kama : Nguo, Vitabu, Maziwa ya watoto, nk. Unaweza peleka vitu hivyo:

Anuani;4203 Wilkens ave, Baltimore MD 21229. 


Pichani Muweka Hazina Jasmin Rubama Akimkabidhi Sister Mariastella Wampembe Pesa Vilizo kusanywa.

  Baadhi ya Watanzania Walioudhuria na Kuchangia kwenye Kikao cha Jana.

3 comments:

Anonymous said...

Mwanzo mzuri! Hongereni Viongozi kwa kazi nzuri.

Anonymous said...

OUT OF TOPIC: jamani muwe mnaangalia na suits za kuvaa kwenye maharusi!! kuchangishwa hukuchangishwa so haukuwa na sababu ya kutonunua suit inayoendana na event!

Anonymous said...

Watu wana uhuru wa kuvaa wanachokipenda kama hakuna dress code. Sorry!