ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 8, 2014

MZEE WA MIAKA 79 AUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.09.2014.
  • MZEE WA MIAKA 79 AUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.
  • MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
  • MAMA MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUTUPA MTOTO NA KUSABABISHA KIFO.
  • MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHENYE MAJI.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MZEE WA MIAKA 79 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GABRIEL MWANDEMWA MKAZI WA KIJIJI CHA IKAMAMBANDE WILAYA YA RUNGWE ALIUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA KIFUANI.

 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 07.09.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IKAMAMBANDE, KATA YA LWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. AWALI INADAIWA KUWA, UONGOZI WA KIMILA KIJIJINI HAPO MNAMO TAREHE 07.09.2014 ULIITISHA KIKAO CHA DHARURA UKIHUSISHA VIONGOZI WA VITONGOJI NA VIJIJI JIRANI NA NDIPO WALIAMUA KUMTAFUTA NA KUMLAZIMISHA MAREHEMU KUHUDHURIA KATIKA KIKAO HICHO NA KISHA KUANZA KUMPIGA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
 MAREHEMU ALIKUWA AKITUHUMIWA KUWA NI MSHIRIKINA KIJIJINI HAPO KWA KUWA ANAWAROGA WATOTO NA KUWA ANAJIPATIA MAZAO MENGI KWA KUWATUMIKISHA WATU KISHIRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE – MAKANDANA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA KWANI MARA BAADA YA TUKIO HILO WALIKIMBIA KIJIJINI HAPO.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADAHARA MAKUBWA KWA JAMII NA KUSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI NA AMEMUAGIZA MKUU WA POLISI WILAYA YA RUNGWE KUWATAFUTA NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WOTE ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MPANDA BAISKELI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ELIBARIKI BARNABA (23) MKAZI WA GOME ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA NAMBA ZAKE ZA USAJILI LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 07.09.2014 MAJIRA YA SAA 18:50 JIONI HUKO UYOLE – JESHINI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
 KATIKA TUKIO LA TATU:
 MAMA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEBORA ERNEST (17) MKAZI WA NTINGA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIKE USIKU WA MANANE NA KISHA KUMTUPA CHOONI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.09.2014 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA NTINGA, KATA NA TARAFA YA MSANGANO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI HOFU YA KUMLEA MTOTO HUYO BAADA YA ALIYEMPA MIMBA KUIKATAA NA NI MKAZI WA NDOLA NCHINI ZAMBIA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA AKINAMAMA KUACHA VITENDO VYA UKATILI VYA KUTUPA WATOTO WACHANGA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA MWENENDO MBAYA WA USTAWI WA JAMII.
 KATIKA TUKIO LA NNE:
 MTOTO WA MIAKA MITATU (03) ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADILIANO FREDRICK MKAZI WA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA ALIKUTWA AMEKUFA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHENYE MAJI.
 TUKIO HILO LIMETOKEA ASUBUHI YA LEO MAJIRA YA SAA 06:30 HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MAREHEMU KABLA YA KIFO CHAKE ALIKUWA AKICHEZA KARIBU NA KISIMA HICHO NA NDIPO ALITUMBUKIA NA KUFA MAJI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUTOA UANGALIZI MZURI KWA WATOTO WAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYO WAZI, KUFUKIA MASHIMO NA MADIBWI YALIYO WAZI KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO.
 Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: