Mdogo wa msanii Side akiwa kwenye picha ya pamoja na Best Nasso, Kigwema na waombolezaji wengine mara baada ya kufika mkoani Lindi.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Best Nasso na Kigwema wamefunguka kuwa daima watamkumbuka msanii mwenzao, Side Boy aliyefariki mapema jana kwa upungufu wa damu katika Hospitali ya mkoa wa Lindi.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu wakiwa njiani kuelekea msibani mkoani Lindi, wasanii hao walisema kuwa watamkumbuka marehemu siku zote kwa kuwa walikuwa marafiki wakubwa ndani na nje ya muziki na kuongeza kuwa ni msanii pekee aliyekuwa akiimba nyimbo zenye meseji zenye kugusa maisha ya watu kwa kujali zaidi ujumbe na siyo soko kama wanamuziki wengine.
“Hakuna neno tutakaloweza kusema kuelezea hisia zetu. daima tutamkumbuka Side Boy kama msanii mwenzetu, rafiki na kaka yetu. RIP”
(Habari/Picha na: Chande Abdallah/Gpl)
No comments:
Post a Comment