ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 3, 2014

LEOLEO HAPANA, LAKINI UNATAKA VOCHA?

LABDA akina dada wataona nimewaandama wao, kwa sababu hata katika toleo lililopita nilizungumza kuhusu wao, nikiwakumbusha kuhusu mambo madogomadogo yanayowashusha thamani katika kujenga uhusiano wao mpya.

Mada yetu ya hapo juu inajielewa wazi. Kuna jambo moja sijui kama na nyinyi mnalifahamu; katika uhusiano wa kimapenzi, mara nyingi wanaume ndiyo huwa na papara sana, wanapenda mambo yaende harakaharaka, wamalize mchezo mapema.

Ni vigumu sana kumkuta mwanaume akawa mvumilivu kwa mwanamke kwa muda mrefu. Kwa mfano, akikutana na mwanamke leo, tuseme katika daladala, madukani au kwenye kinywaji, wakishapeana namba za simu, mawasiliano huanza mara moja.


Na katika mawasiliano hayo, ndiye atakuwa wa kwanza kuhimiza kuhusu kukutana, kwa ajili ya kufahamiana zaidi na ikibidi kumaliza mchezo kabisa. Hapa ndipo panapokuwa patamu, kwa sababu ya mazoea pia kutuonyesha kuwa wanawake ni wagumu kidogo kukubali haraka wito wa kukutana na wenza wao wapya.

Wanawake wana kawaida moja, wanapenda haraka lakini wagumu kuamini. Wanaweza kumpenda mkaka, iwe kwa muonekano wake, uongeaji wake na hata kwa uwezo wake kifedha labda, lakini ni wazito kidogo kuamini kama penzi lao linakwenda sehemu sahihi.

Mazoea haya yanaonyesha kuwa wanahitaji muda kidogo wa kujiridhisha, wanataka kuamini kama wanapokwenda ni mahali sahihi, mtu wanayekwenda kushirikiana naye kimapenzi ni mwenyewe? Maana wao wana msemo wao unaowatisha sana, kutendwa!

Wanaogopa kutendwa. Mara nyingi tu utawasikia, sitaki tena mwanaume, nimeshatendwa! Na uzoefu huu unaonyesha pia kwamba wanawake ndiyo wanaoumia zaidi uhusiano wao unapoisha, hasa kwa kutofautiana kuliko wanaume.

Wababa wengi hawanaga maumivu ya kweli uhusiano unapovunjika, labda kama anayeondoka ni mkewe au mama wa watoto wake, ingawa hata hivyo, maumivu hayawi ya kiwango kikubwa.

Sasa baada ya kutoa muhtasari huo, ngoja sasa nizungumzie tabia hasi ya wanawake kuelekea kwenye huo ujenzi wa uhusiano mpya. Sina uhakika kama suala hili ni la miaka mingi, kwa sababu teknolojia imebadilika katika miaka ya hivi karibuni.

Hapo mwanzo nimesema kwamba wanaume wana haraka, wanawake wanasita ingawa kimtindo wanakuwa wamekubali. Sikiliza simulizi ya Tony, kijana aliyenilalamikia tabia asiyoipenda ya wanawake.
“Nina kawaida ya kupiga piga namba ovyo bila kumjua mwenyewe, lengo langu ni kutafuta mwanamke ambaye naweza kujenga naye urafiki wa kimapenzi.

Nikipiga, akipokea mwanaume namwambia samahani, wrong number, akipokea pia mwanamke namwambia hivyohivyo lakini hapa nitaanza kumtumia meseji.
“Nimefanya huu mchezo kwa muda mrefu na kwa kweli nimefanikiwa kuwapata wanawake kama watatu kwa staili hii. Nachat nao lakini baadaye ninamuomba urafiki wa kawaida na baadaye naomba wa kimapenzi.

“Wapo ambao huanza kuwaomba urafiki wa mapenzi moja kwa moja. Kuna kitu kimoja nimekigundua katika hizi harakati zangu. Wanawake ni wagumu sana kukubali kushiriki tendo siku ya kwanza kukutana, lakini sasa, ni wepesi kweli kuomba vocha na nauli.

“Utakuta anakuambia leoleo hapana, lakini hapohapo atataka umnunulie vocha au umpe hela ya nauli. Ndiyo maana nikaomba uwaulize, kwa nini hawawezi kutoa penzi leoleo, lakini wanataka vocha leoleo?”
Hiyo ndiyo simulizi ya huyu kijana, Tony. Sina uhakika kama anachosema ni kweli, kwa sababu sijajua dada zangu na mbwembwe zao. Inawezekana ikawa ni baadhi yao, kwa sababu tabia ya Abdalah, haiwezi kuwa ndiyo ya wanaume wote!

GPL

4 comments:

Anonymous said...

Naungana na ndugu yangu abdalah yamenikuta miye sana tu ni 90% ya wana wake wana mchezo huo utaanza kumpa anachotaka halafu baadaye anakwambia yeye ana bwana ake halafu wanajisifu kwa wenzie kuwa ana Buzi lake hapo sasa ndiyo maana wanaumme nao wamemka tunawatenda tu ..

Unknown said...

Kweli lakin

Unknown said...

Kweli lakin

Unknown said...

Kweli lakin