1. Mwanangu, mwanamke anaweza
kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa
mama wa watoto wako, lakini ukipata
mwanamke ambae atakuwa kama
mama kwako, mama kwa wanao na
mama kwa familia, tafadhali mwanangu
usimuache huyo!
2. Mwanangu, usimfanye mwanamke
wako kuwa ndio wa kupika na kufanya
kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo
sio nzuri Kwani hata nyakati zetu,
mashamba yetu yalijulikana kwa majina
yetu wanaume lakini tulifanya kazi
3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni
kichwa cha familia, simaanishi kutuna
kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi
yako, angalia kama utaona tabasamu
usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu
katika ndoa na haileti ukuu wa familia!
4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha
marefu na ukapunguza misongo ya
mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti
ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo
awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya
kila siku ya familia kwa kumkabidhi
fungu husika hata kama limetokana na
michango yenu wawili. wanawake
wanajua sana kupanga bajeti na hii
haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia
hela hovyo wakati akijua kuwa
nyumbani kuna mahitaji ya msingi,
lakini hela zikiwa mikono mwako
ataendelea kuomba hata kama utakuwa
umeishiwa!
5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga
mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani
ya moyo wake kwa muda mrefu sana
na huacha kidonda ambacho hukawia
sana kupona. Ni hatari sana kuishi na
mwanamke mwenye majeraha moyoni!
6. Mwanangu, sasa unaamua
kuoa,kama bado utaendelea kuishi
maisha kama ya ubachela na mke
wako, sio muda mrefu utakuwa
bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi
maisha ya mke na mume!
7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake
wengi na watoto wengi kwa sababu
tulikuwa na mashamba makubwa na
mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa
sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo
mkumbatie mwanamke wako peke yake
kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya
watoto ni makubwa sana. Angalia
ukubwa wa familia yako!
8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao
nilikuwa nikikutana na mama yako
inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa
nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu
pekee tulichoweza kufanya chini ya
mwembe ilikuwa ni kukumbatiana
pekee.nakushauri ukikutana na
marafiki wa kike kikubwa unachoweza
kufanya nao ni kupeana mikono na
ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio
vinginevyo!
9. Mwanangu, usibadilike mara
utakapoanza kupata mafanikio Zaidi,
kuliko kuwahudumia hao viruka njia
wa mtaani ambao hawajui mmetoka
wapi na mkeo, nakushauri utumie na
kufurahia mafanikio yako na mkeo
ambae aliweza kusimama imara wakati
wote wa mapito yenu magumu.
10. Mwanangu, kumbuka unapoanza
kusema au kuona mke wako kabadilika,
ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa
ukikifanya umeacha kukifanya.
Jitathmini na anza kufanya au kutimiza
wajibu wako.
11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha
au kumlinganisha mke wako na
mwanamke mwingine wa nje, kwani
hata yeye anakuvumilia sana na
hajakufafanisha na mwanaume
mwingine yoyote huko nje na ndio
maana aliamua kuwa na wewe.
12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu
kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama
mwanamke anasema ana haki sawa na
wewe katika nyumba, basi gawanya
mahitaji yote ya ndani kwenu katika
sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza
nusu yako na mwambie atimize nusu
iliyobaki.
13. Mwanangu, nilimuoa mama yako
akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa
naenda sana kwao kabla sijamuoa,
lakini kutomkuta mkeo bikra
kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa
muhuni, kumbuka wanawake wa enzi
zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua
mwenyewe na ukigoli wake hukuujua
kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya
ndoa kwenye ndoa yenu.
14. Mwanangu, sikuwapeleka dada
zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga
kama wazee wengi wa hapa kijiji
wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga
huu, kwani kiwango cha mafanikio ya
wanawake sasa kimefanya wanaume
waonekane ni watu wa kawaida sana
na sio muhimu kama enzi zetu.
Ukijaliwa watoto wape elimu.
15. Mwanangu, zamani enzi za ujana
wetu, wanawake walikuwa na urembo
wa asili, ingawa siwezi kukudanganya,
wengine waliongeza urembo kwa
kujichora hina na hata kutoboa pua na
masikio lakini usisahau hawakuonyesha
maumbile yao nyeti hadharani kama
sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!
16. Mwanangu, mama yako na mimi
hatuna hisa katika kila kitu
kinachoendelea kwenye maisha yenu,
jaribuni kutatua changamoto zenu
wenyewe bila kila mara kuja kwetu
kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na
ukomavu wa kutatua changamoto zenu
bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.
17. Mwanangu,nilimnunulia mama
yako kifaa cha kupikia vitumbua ili
aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia
nilimsaidia kununua cherehani yake ya
kwanza, tafadhari msaidie mke wako
kutimiza ndoto zake kulingana na
uwezo wako kama ambavyo
unahangaika kutimiza ndoto zako.
18. Mwanangu, usiache kutusaidia
mimi na mama yako, utu uzima una
changamoto nyingi sana na Mungu
akikujalia utaziona muda ukifika.
Pamoja na kutimiza majukumu yako
kama baba wa familia kumbuka pia
bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.
19. Mwanangu, kila upatapo muda wa
kusali, Sali na familia yako, kuna kesho
ambayo huijui, ongea na MUNGU wako
ambae anajua kila kitu kila siku!
20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA
NDOA MWANANGU….NAKUPENDA!
3 comments:
"Ndoa ni pamoja naukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu."
NAWEKA MSISITIZO TU
AMEN!!!
mwanamke hapigwi fimbo anapigwa kwa kanga.
Post a Comment