Advertisements

Monday, September 22, 2014

NINI CHA KUFANYA MPENZI WAKO ANAPOWASILIANA NA EX WAKE?

Kabla sijaingia kwenye mada ya leo, hebu tushirikishane kuhusu hali iliyomtokea dada yetu mmoja kutoka jijini Dar es Salaam. Aliwasiliana nami siku kadhaa zilizopita, akiwa analia, amekata tamaa, anaomboleza mithili ya mtu aliyepewa taarifa za msiba. Alichokisema ni hiki:

“Nimeishi na mume wangu kwa miaka kumi na tumejaliwa kupata watoto watatu. Huyu wa mwisho ana umri wa miezi saba, nilimzaa mwanzoni mwa mwaka huu. Kilichonifanya nipige simu, nimegundua kwamba mume wangu anawasiliana na mpenzi wake wa zamani aliyekuwa naye kabla hatujaanzisha uhusiano wa kimapenzi (ex wake).

“Nimefuma meseji za kimapenzi, wanachat wakionesha dhahiri kwamba kila mmoja bado anampenda mwenzake. Yaani mume wangu anamtamkia maneno matamu ambayo hata mimi hajawahi kunitamkia. Nimechanganyikiwa, natamani kunywa sumu nife lakini kila nikiwaangalia wanangu, hasa huyu wa mwisho najikuta nikibadilisha uamuzi.

“Naiona dunia chungu, nahisi nimebeba mzigo mzito kuliko uwezo wangu,” alisema dada huyo huku akiendelea kulia kwa uchungu. Hebu jiweke kwenye nafasi yangu, utamshauri nini dada huyu? Najua kila mmoja analo jibu lake ndiyo maana nikaileta mada hii mezani.

Nataka tujadiliane na wewe msomaji wangu, unapogundua kwamba mpenzi wako, mchumba wako au mume/mke anawasiliana na mpenzi wake wa zamani, nini cha kufanya?
Kabla ya yote, ni lazima ujue kwamba hakuna jambo gumu kama kuachana na mpenzi ambaye mliwahi kupendana, mka-share pamoja vitu vingi katika maisha yenu, bila kujali sababu iliyofanya mkaachana.

Wengi huachana na wapenzi wao wakiwa bado wanawapenda, matokeo yake wanapoingia kwenye uhusiano na mtu mwingine, taratibu huanza kurudi kule walikotoka, jambo ambalo husababisha maumivu makubwa kwa anayetendewa jambo hilo.

Kabla hatujaangalia nini cha kufanya unapogundua mpenzi wako anawasiliana na mpenzi wake wa zamani, tuanze kwa kuangalia mbinu za kumgundua mpenzi wako kama anaendelea kuwasiliana na mpenzi wake wa zamani.

UTAGUNDUAJE KAMA BADO ANAMPENDA?
1. Anamzungumzia mara kwa mara. Hii ni dalili ya awali ya mtu ambaye bado anawasiliana na mpenzi wake wa zamani. Mara kwa mara atakuwa akimzungumzia katika maongezi yenu bila hata sababu za msingi. Atakuwa akipenda kumtolea mifano, iwe mizuri au mibaya.

GPL

1 comment:

Anonymous said...

HOW OLD ARE YOU AND WHEN DID YOU START YOUR POLITICAL CAREER?