ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 9, 2014

Ntagazwa agaragazwa na Mzanzibar Uchaguzi Chadema


Arcardo Ntagazwa.
Na Mwandishi wetu
KWA mara ya kwanza historia imeandikwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumchagua mzanzibar Hashimu Juma Issa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza kutoka Zanzibar.
Hashimu alishinda katika mzunguko wa pili kwa kura 47 na kumzidi mpinzani wake Arcardo Ntagazwa aliyepata kura 22 kati ya kura 71 zilizopigwa na wajumbe, kura mbili kuharibika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chadema, Issa alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake aliochaguliwa nao, hatahakikisha Chadema inaingia Ikulu ya Tanzania Bara na Zanzibar.
“Tunawashukuru wajumbe waliotuamini na kutuchagua… tuna mwaka mmoja wa kufanya kazi ya kuipeleka Chadema Ikulu ya Bara na Zanzibar hivyo kwa kusaidiana na wenzangu tutahakikisha ushindi huo unapatika”
“Namshukuru sana mwenyekiti wangu Mbowe na Katibu wa chama Dk. Slaa kwa kukieneza chama kwa kasi bara … sasa nawaahidi kwamba nitahakikisha nitakieneza Zanzibar kama ilivyo huku” alisema Issa
Mapema akitangaza majina hayo, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda Benson Kigaila, alisema uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti iliyokuwa na wagombea watano ulishindwa kumpata mshindi katika mzunguko wa kwanza baada ya kukosa aliyepata asilimia 50 za kura zote.
“Katika mzunguko wa kwanza ArcadoNtagazwa alipata kura 23, Hashim Juma Issa (36), Jacob Qorro (0), Jomba Koyi (15) na Kayaga Ismail Kayaga (3) …ikawalazimu kurudia mzunguko wa pili kwa wagombea waliopata kura nyingi na hatimaye kumpata mshindi”
Katika matokeo yao, Kigaila alisema nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara alipata Susan Lyimo aliyepata kura (51)na kuwashinda wapinani wake Clavery Ntidicha (05), Omary Juma Mkama (13) na Othman Haule (05).
Kwa upande wa Zanzibar aliyeshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa ni Omar Masoud Omar (42) na kumshinda mpinzani wake Bikwao Hamad Hamis (32),.
Kigaila alisema nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa na mgombea mmoja Rodrick Lutembeka ambaye alishinda kwa kura 69 kati ya kura 74, zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo na tano ziliharibika.
Aloisema nafasi nyingine ambayo ilikuwa na gombea mmoja ni ya Mweka hazina ambayo ilichukuliwa na Erasto Gwota aliyeshinda kwa kwa kura 58 kati ya kura 75 zilizopigwa na wajumbe wakati kura 17 zilimkataa.
Waliofanikiwa kushinda nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Chadema ni Victor Kimesera, Florence Kasilima, Alfred Ntupwa na Hugo Kimaryo na kwa upande wa Zanzibar aliyepita ni Haji Ussi Haji.
Kigaila alihitimisha kwa kuwataja wajumbe walioshinda kuingia katika mkutano mkuu ni Charles Kikomingo, Mary Jumbe Nakoe, Mery Florian Joachim, SylevesterShirima, Timothy Kirway na William Mwangwa wakati upande wa Zanzibar waliopita ni Hassan Ame Kheri, Khatibu Ali Khatibu, Haji Kali Haji na Rashid Omar.
Akitoa maazimio matatu ya mkutano huo, Katibu Mkuu mpya (Lutembeka) alisema wazee wa baraza hilo wameitaka serikali kutangaza haraka tarehe ya uchaguzi wa serikali za mtaa.
Maazimio mengine ya mkutano huo ni kuunga mkono uamuzi wa wajumbe wa chama chao kwa kujiunga na wenzao na kuanzishaUmoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuitaka tumeya uchaguzi kutangaza mara moja ratiba ya uandikishaji wa daftari la kupiga kura

No comments: