ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 30, 2014

NYUSI AKUTANA NA WANAMSUMBIJI WA ZANZIBAR

Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akizungumza na Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wampigie kura kwani amekuja na mikakati mizuri ya kuboresha uchumi ambapo amedhamiria kuiondoa Msumbiji kwenye orodha ya nchi masikini,pia aliahidi kuwawezesha wakina Mama wa Msumbiji.
Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar wakisikiliza sera za Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi kwenye mkutano uliofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar Asilia Lunji baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni kwa wapiga kura wanaoishi Zanzibar,Nyusi aliwaambia kuwa amefanya mkutano wa kwanza nchini Tanzania kwa sababu ya mahusiano mazuri baina ya Msumbiji na Tanzania
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi mara baada ya mgombea huyo kumaliza ziara yake Zanzibar.
Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiwaaga wananchi wa Zanzibar

No comments: