Mungu mkubwa! Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ kisha kunusuriwa, super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, hatimaye mambo yameanza kumnyookea baada ya kulamba shavu tenda nono ya kulisha Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa Wikienda, Ray C almaarufu Kiuno Bila Mfupa amefungua bonge la ‘restauranti’ maeneo ya Mwananyamala Hospital, ambapo amepata tenda ya kuwahudumia chakula wafanyakazi wa hospitali hiyo na Idara ya Maji (Dawasa) ambapo anafanya kazi hiyo kwa saa ishirini na nne na muda mwingi anakuwepo yeye mwenyewe.
“Bidada sasa hivi yupo njema sana. Kalamba shavu la kulisha Hospitali ya Mwananyamala na Dawasa na hapo ni mchana na usiku so yupo bize kinoma.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu waliusaka mgahawa huo na kufanikiwa kuupata ambapo walimkuta Ray C akiwa bize kuhudumia wateja ambapo alisema: “Namshukuru Mungu kwani nimepata tenda ya kuwapikia chakula wafanyakazi wa Mwananyamala na wale wagonjwa ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya.”
No comments:
Post a Comment