ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 6, 2014

TANGAZO MAALUM- HALI YA JUMUIYA YETU - DMV



Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania hapa Washington DC, Maryland and Virginia Unapenda kuwataarifu wanajumuiya kuwa hakuna Mahakama yeyote iliyosimamisha shughuli au mikutano ya jumuiya. Ombi la kusimamisha shughuli za jumuiya lilikataliwa na Mahakama na malalamiko mengine yaliyowasilishwa mahakamani yanajibiwa na Mwanasheria na yatawasilishwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria na wakati uliotolewa na Mahakama.

Hivyo basi shughuli za Jumuiya zitaendelea kama kawaida kwa mujibu wa katiba yetu na tutawajulisha maamuzi ya mahakama mara tutakapopata majibu. Mkutano mkuu wa Jumuiya kwa mujibu wa katiba ya Jumuiya utafanyika kama ulivyopangwa Jumapili September 7, 2014, kuanzia Saa 11:00 Jioni. (5:00PM).

Tunawakumbusha kulipia ada yako kama bado hujalipia ili uweze kuchangia mawazo katika maendeleo ya Jumuiya yetu.


Viongozi wanawahakikishia Wanajumuiya kuwa usalama utakuwepo.

MTU YEYOTE ATAKAYELETA FUJO AU KUHATARISHA USALAMA WA MKUTANO WA JUMUIYA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

UONGOZI


3 comments:

Anonymous said...

DMV jamani, I thought mlikuwa manaishi kama vijiji vya Ujama, it seems kuna matatizo makubwa kubwa. Can't this be resolved kwa kukaa pamoja na kuzungumza kama watu wakubwa.

Anonymous said...

purpose or organisation
Our motto is 'Promoting Unity among Tanzanians in Washington DC, Maryland and Virginia regardless of peoples' religions, political affiliations or genders.

Hiii inakuwaje hapa?

Anonymous said...

Mkawaulize TEAM libe waliokwenda MAHAKAMANI!! ITS PATHETIC, IMAGINE NDIYE ANGESHINDA URAIS!! MUNGU KWELI KATUEPUSHA NA BALAA HILI HATA KURA YANGU NILIYOMPA NAJUTA HE WILL NEVER GET THAT VOTE FROM ME!!!

Kitu cha kujitolea kinataka kuingiza jumuiya na mahakama za marekani???? Sijawahi kusikia duniani in any community....Na bora wameenda huko mahakamani NA WAKISHINDWA WATAKUJA NA LINGINE. Hawana cha kufanya wajameni???? Tired and Sick reading this news