Uongozi
wa Jumuiya ya Watanzania hapa Washington DC , Maryland
and Virginia Unapenda kuwataarifu wanajumuiya kuwa hakuna Mahakama
yeyote iliyosimamisha shughuli au mikutano ya jumuiya. Ombi la kusimamisha
shughuli za jumuiya lilikataliwa na Mahakama na malalamiko mengine
yaliyowasilishwa mahakamani yanajibiwa na Mwanasheria na yatawasilishwa
Mahakamani kwa mujibu wa sheria na wakati uliotolewa na Mahakama.
Hivyo
basi shughuli za Jumuiya zitaendelea kama kawaida kwa
mujibu wa katiba yetu na tutawajulisha maamuzi ya mahakama mara tutakapopata
majibu. Mkutano mkuu wa Jumuiya kwa mujibu wa katiba ya Jumuiya utafanyika kama
ulivyopangwa Jumapili September 7, 2014, kuanzia Saa 11:00 Jioni. (5:00PM ).
Tunawakumbusha
kulipia ada yako kama
bado hujalipia ili uweze kuchangia mawazo katika maendeleo ya Jumuiya yetu.
Viongozi wanawahakikishia Wanajumuiya kuwa usalama
utakuwepo.
MTU YEYOTE ATAKAYELETA FUJO AU KUHATARISHA USALAMA
WA MKUTANO WA JUMUIYA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
UONGOZI
3 comments:
DMV jamani, I thought mlikuwa manaishi kama vijiji vya Ujama, it seems kuna matatizo makubwa kubwa. Can't this be resolved kwa kukaa pamoja na kuzungumza kama watu wakubwa.
purpose or organisation
Our motto is 'Promoting Unity among Tanzanians in Washington DC, Maryland and Virginia regardless of peoples' religions, political affiliations or genders.
Hiii inakuwaje hapa?
Mkawaulize TEAM libe waliokwenda MAHAKAMANI!! ITS PATHETIC, IMAGINE NDIYE ANGESHINDA URAIS!! MUNGU KWELI KATUEPUSHA NA BALAA HILI HATA KURA YANGU NILIYOMPA NAJUTA HE WILL NEVER GET THAT VOTE FROM ME!!!
Kitu cha kujitolea kinataka kuingiza jumuiya na mahakama za marekani???? Sijawahi kusikia duniani in any community....Na bora wameenda huko mahakamani NA WAKISHINDWA WATAKUJA NA LINGINE. Hawana cha kufanya wajameni???? Tired and Sick reading this news
Post a Comment