ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 6, 2013

WATANZANIA WA NEW YORK, NJ, CT NA MA MNAKARIBISHWA KWENYE SHEREHE ZA UHURU DECEMBER 7, 2013 KUNYWA KULA NA KUCHEZA HADI MAJOGOO.

Watu wote mnakaribishwa siku hii ya uhuru kutakuwa na vyakula, vinywaji music na mambo mengi ya kuchangamsha. Unachotakiwa ni kulipa 30$ tu mlangoni njoo tusherekehe siku yetu watanzania kufika kwenu ndiyo mafanikio ya sherehe hii. Sherehe zitaanza saa 11 na nusu jioni njoo mapema uwahi meza yako, usije kula chakula na kunywa ukiwa umesimama chakula kikakimbilia miguuni na ukashindwa kucheza music. Ma DJ wetu bora watatuchezesha mwendo wa ndombolo na rusha roho hadi kukuche, vaa kiafrica kuonyesha uzalendo Wote mnakaribishwa. Ukitaka kufika kwa kutumia train chukua N, Q kwenda Queens  hadi 36Th Street, Na tembea mtaa mmoja hadi 37Th St kunja kulia jengo litakuwa mkono wako wa kushoto.
Ticket zimeanza kuunzwa mbele ya desk la Tanzania Mission New York. Na pia unaweza kupa ticket hizo kupitia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo ya uhuru, kwa kupiga # hizi za simu, #347 663 0781, #917 557 3195, Pata ticket yako sasa.
 Address
 Claudio's Cafe II,
 32-23 37th Avenue. 
Astoria, NY 11101
Siku hiyo ya Uhuru wa Tanganyika kutakuwa na Nyama choma kutoka kwenye jiko la kisasa la Temba Engineering Service. Jiko linalochoma nyama kwa kiwango cha hali ya juu kabisa, njoo na uonje nyama iliyochomwa na jiko hilo la kisasa linalotumia computer maalumu inayokujulisha kuwa nyama imewiva kwa kiwango kinachotakiwa kuliwa na binadamu bila kuleta madhala yeyote.
New York Tanzania Tema wako fit kwa mchezo.

Uwanja ni huu utakaomaliza ubishi  wa mchezo wa kirafiki kati ya New York na New England (Umoja) Springfield Boston hapa New York wachezaji kuwahi mapema mchezo utaanza saa 8 mchana.   Katika uwanja wa 

Aviator Sports And Event Center 
Address 
3159 Flatbush Avenue ,
 Brooklyn.Ny 11235. 
Team ya New York baada ya kujifua sana huu ni mchezo wao wa kwanza, wachezaji wamejipanga vizuri ili kuwafundisha mpira team ya Springfield. Baada ya majigambo ya pande mbili kila mmoja akisema ni zaidi ya mwenzie sasa siku ya uhuru jumamosi ya tarehe 7 mzizi wa fitina unakatwa, ukisikia PAHHHHHHHHH labda itokee tuuuuuu!!!

28 comments:

Anonymous said...

kwani uhuru tumepata sisi watanzania na uhuru huu ni wa wadanganyika au wasote pamojana na wazanzibari tuwekeni wazi jamani na hongereni sana kwa kuweka kitu adimu kama hichi mambo muruwa kuserubeuka hadi majogoo lakini tujiulize je tumepata uhuru kweli au uhuru wa bendera

Anonymous said...

UHURU HUU UNAFAIDA GANI KWETU KAMA BADO TUNATAWALIWA NA KUWA OMBA OMBA KILA SIKU WAKUU WETU VIJISAFARI VYA MAJUA VYA HAPA NA PALE KUOMBA TONGE.

TUAMKE WATANZANIA TUSIWE WAJINGA WAJINGA JENGA UHURU WAKO NA FAMILIA YAKO NDO CHA MUHIMU MAISHA YANAKWENDA HAYARUDI NYUMA UMRI UNAPOTEA WATOTO WANAKUWA NA WEE MTANZANIA MTU MZIMA UNATAKIWA UKUWE NA KUJUA THAMANI YAKO NA NCHI YAKO INA UHURU GANI

Anonymous said...

uhuru wa watanganyika si wa zanzibar bado tunatafuta uhuru wetu

Anonymous said...

kama vipo vya bure nitakuja sijali uhuru wa nani wala nani hainihusu burudani ndo inayonihusu na kukimbiza damu yangu katika mwili wangu hongereni waandaji wa party tunakuja kusherehekea michongo chongeni msituyayushe wapinga boxi chongeni mtatafuta pesa na mtaziacha hapa hapa njoeni tushereheke msidijai kujua sana siasa za uhuru

Anonymous said...

Huyo mjinga nchi ya kuomba yes ndiyo thard world ulitaka asisafiri akae tuu ?? Wacha ujinga wewe joto hasira una point

Anonymous said...

Anoy wa Novemba 15 saa 7:27pm kakwambia nani BURE? dola $30 ndio unapata chakula na vinywaji!

Anonymous said...

Poa. Mi Nipo tayari kununua ticket. Nitakupatia wapi?

Anonymous said...

faida ya kusafiri wakuu wetu ni nini na uhuru huu unafaida ya nani hizo pesa wanazo safiria hawa wakuu wetu na deligation zake si zingekaa na kuwasaidia waalala hoi nyumbani wacha ujinga anonymous wa november 16 at 3;45 naona wewe ndo wamoja wao mnaokula hii nchi kwa meno yenu yote na jamaa zenu kuendeleza ufisadi halafu eti third world ndo maana tutakufa na kuwa third world forever kwa tamaa mbele mauti nyuma ufisadi wenu umezidi ndo maana wazungu wanakuuweni wameshajua mnapenda pesa na si kutetea nchi yenu na uhuru wenu

Anonymous said...

Sasa ninyi mnaolalamika, mnataka watu waomboleze uhuru?????????

Anonymous said...

Busara ni kitu muhimu ktk maisha na ambacho hakihitaji mtu kwenda shule. Matusi katika kujenga hoja ni upungufu mkubwa wa fikira katika kuisaidia au kuelimisha jamii husika. Tangazo limetoka kuijulisha jamii husika kuwepo kwa tukio muhimu la kihistoria. Na endapo umeona kuna umuhimu wa kushiriki au kutoshiriki hili ni uamuzi wako binafsi ambao jamii husika haipaswi kujua. Tujitahidi kuchangia hoja endelevu kwani wanaosoma ni watu wa rika tofauti na wanapaswa kujifunza au kupata uelewa kutokana na hoja zinazochangiwa.
Jumuiya Oyeee...Oyeeee.
Zidumu jumuiya za Watanzania
Asanteni
Mdau.

Anonymous said...

ukienda shule siyo kama una busara wengi tu wamekwenda shule na hata hatuzioni busara zao kuwa na busara ni kuelimika na kutaarabika.
nikweli uliyosema wengi wanasoma blog hii na tuwe wakweli katika kizazi chetu tuwaelimishe siyio vipati pati bila mpango watu hata maana ya uhuru hawaijui hata ukiwauliza uhuru ulipatikani lini tarehe gani na waliopigania uhuru mpaka hivi sasa sisi tunausherehekea ni wakina hawaujui.

sina nia ya kuchafua blog hii kwa party yenu adhimu lakini busara kitu adhimu sana na kwenda shule si hoja wako wasiokwenda shule na wwana akili kupita waliokwenda shule kwa kupata vikaratisi vya hapa na pale vya diploma uchwar uchwra ha kujidai wasomi.

partini lakini pia muwaelimishe watu nini maana ya uhuru sio kunywa mipombe ovyoo na kusaza vyakula na kujidai wasomi mchwra kumbe pumba tupu kichwani

mkifanyiwa mitihani ya civics ya uhuru wenu hata kuujua hamuujui aibu kubwa what a waste and shame.

nendeni mkajiserebuwe wajanja wajajaruke mapocho wapochoke zaidi

jumuiya za watanzania zidumu zidumu kama fikra za ccm oyeaaaa ha ha ha

Anonymous said...

aisee nani kakwambia bwana watu wahusunike katika sherehe zenu za uhuru lakini muwe na busara na hekma na kwenda shule siyo kama unabusara au ndo msomi.
tunachosema hapa ni hivi enzi za zamani za ujinga ujinga watu kutokaa na kutafakari na kufikiri umepwita na wakati labda kwa mapocho ndo watakao ona sawa na wenye faida zao hamkatazi msisherehekea au ku party na kusazaa mpaka liamba cha muhimu waelimisheni wenzenu uhuru huu umepatikanaje wakina nani walipigania uhuru etc na toka tupate uhuru matunda yake yako wapi serikali inafanya nini kwa walalahoi huko nyumbani na huku tulipo sisi majuuu.

ni hicho tu hatuna niamba mbaya kuponda jitihada za wanakamati za kufanya sherehe za uhuru lakini binadamu kia unapoishi akili inakuwa hasinyai labda kama ndo unazeeka vibaya.

na wala hatusemi kwenye hizo party zenu watu wawe darasani wanasoma huo uhuru muwe mnawafundisha huku mnaserebuka mpaka liamba majongoo no hatowezekana lakin tunachosema ni hivi

muwe mnawapa watu civic classes wajui huu uhuru wao na toka uhuru wao tumefaidika na nini na sisi tunafanya nini kama watanzania kusaidia huu uhuru wetu siyo kujifaragua kwa ku party bila mpango.

mwenye busara na hikma atatambua nasema nini aliyepocho na mkaidi na kwa manufaa yake na anachokipata katika hii party atakanusha

heko wanakamati wote kwa party hiii tutakuja tuje tujionea mambo dunia ndo hii kuserebuka serebuka bila busara na hekma na kwenda shule si yo deal deal kupata na kuelimika kwa kila siku unavyoishi na kupumuwa na kumshukuru mola wako.

Anonymous said...



msije msije vishoka vya kupiga maboksi kaeni pigeni maboksi halafu muende job inginewe tena mpige maboksi ndo mlichokijia marekani pigeni maboksi yenu wee mpake mtoke roho zenu na kuzeeka bila mpango msije kwenye uhuru wetu wacha tuserebuke wenyewe kwanza wabahili wakubwa wakutoa pesa zenu mtakufa nazo hizo mnatuchafua bwana na wewe luke usiweka comment za hawa wachovu wapiga maboksi hawajui starehe zaidi ya kwenda makazini kupiga maboksi na njaa zao

ohaa njoeni wangwana wenye kumudu kulipa kiingilio mpate burudani poa wasio taka waende wakapige maboksi na ubahili wao na watoke roho zao

Anonymous said...

Anonymous Anonymous said...

tumeka na kujiuliza baada ya starehe hizi nini maana ya uhuru wa nchi yetu na faida zake na hasara zake kwa wananchi wote hasa hasa wa vijijini waliopo nyumbani.

au basi tunasherehekea tu bila kutafakari huu uhuru wetu na kizazi chetu.

tukuwe watanzania tuwe watu wa kufikiri na kuona mbali sio wafikiriwa

shukran

Anonymous said...

Bad neighbourhood siendagi .nisije pigwa bunduki bureee.Wengine tumezaliwa na kukulia Masaki .Queens ni Kama kariakoo na kariakoo kuna nafuu.Wasije wakaharibu my Bentley

Anonymous said...

We bad neighbourhood unaijua au majungu tuu yamekuzidi. ..kwani umelazimishwa kuja mijitu mingine sijui imetoka wapi. ..can't wait December 7tuka serebuke.

Anonymous said...

watu wenginewe bwana wanajifanya kujua sana kumbe majuha eti tumekulia masaki ukichungu utaona wazazi walitoka vijijini mikoa minginewe wakaja dar na hivyo viposti vya kuajiriwa na serikali ndo vikawapa nafasi ya kuishi huko masaki eti queen ni kama kariako

unaijua kariakoo wewe, wakuja wote wakitoka mikoani wanashanga wakiifika kariakoo na ndo maana hawataki kurudi vijijini mwao kwa neema ya kariakoo na mtu anayeishi new york kama hajui queens basi ni mshamba ile mbaya eti bad neighbourhood wee new york yenyewe toka umetoka huko kwenu kijiji ukatuwa dar na kupata nafasi ya kuishi masaki imekuwa nongwa na kuja huku marekani uka kaa huko matokomeyani shambani ndo unajiona msataarabu unaaa saa kumi na mbili kama jogo wa shamba huko upstate unajidai bad neighbor hood.

ukitaka kuwajua watu washamba na wajinga basi ndo kama hawa kuponda sehemu toka atoke kwao kijijini kutowa marekani manhattan hajui queens hajui haafu anajidai misifa sifa yake

baba leloooooooo usije usije kwani unalazimishwa shoga mkubwa wewe ungekuwa mwanamme kijume cha mbegu usikeropoka ropoka kama demu

Anonymous said...

New york city Tanzania community oyeeeh tutakuja kwa wingi kusherekea uhuru wa inchi yetu#proudTanzanian

Anonymous said...

UHURU MY FOOT TUPA HUKO LABDA KAMA HUNA KAZI YA KUFANYA. NONESENSE

Anonymous said...

wewe mdau unayetoa mfano wa "masaki" unaonekana DAR TRANSIT na hukai na wala hujafika NYC. Queens utakuwa umeisikia kwenye movie ya Eddie Murphy "Coming to America" ambayo inavyoonekana umeiona few days ago…Bentley my foot. na kama kweli ungekuwa unajiamini ungeandika jina lako la ukweli….Pumbafuuuuuuuuu

Anonymous said...

Hahahahahaha...Lol we mshamba kweli umetokea kijiji gani mpaka unapaita Queens kariakoo. ..kwanza hamna mbongo mwenye Bently New york city wadanganye wengine unaendesha mkoko huko Lol. ..kama huna $30 sema tukutolee uje userebuke wewe.

Anonymous said...

Inakuwaje Flaviana Matata anakaa Harlem NYC anaenda DC kwenye sherehe hizi badala ya kusherehekea na nyie wa new yorker?

Anonymous said...

Hey vijimambo team hivi kwanini kila kukiwa na shughuli za wa Tanzania wengine wanatoa hoja zavitisho kama huyu anaeogopa kupigwa risasi mwengine akiona si ataogopa kuja na nyinyi mnazitoa hoja kama hizi sehemu ni Astoria queens upande mwingine wa Manhattan

Anonymous said...

Flavian Matata hatuja muona kwenye sherehe zote za watanzania hapa new york na wala hatuzuii kufanya shuhuli zetu,,ingekuwa kiongozi wa serikali hapo sawa, muache afurahi kivyake na sisi kivyetu haina shida

Anonymous said...

No mdau wa Dec 4, 2013 una miss the point, Flaviana Matata ni Mtanzania anayefanya vizuri hapa Marekani kwenye mashughuli yenu kama haya inatakiwa kum "book" na kulipia appearence yake, sasa jumuia ya wabongo New York mnafanya mambo kiswahili wajanja wa DC wamewazidi akili! kubalini yaishe

Anonymous said...

afadhali mmeandika sherehe ya uhuru wa tanganyika nimefurahi sana kuona jambo hili thank you guys hivi ndo ilivyokuwa inatakiwa mfanye

Anonymous said...

watu wa new york ndo kwanza wanaanza mambo haya jamani wapeni time sawa kama wa dc wameyafanya haya longtime sawa si mbaya hata kinyonga anakwenda kwa miguu yake lakini si aanafika so maneno maneno ya nini na asiyetaka kuja halazimishwi jaamani dc watu hawako busy sana kama new york wana free time sana za kuka kwenye vijiweni etc ndo maana mapati mapati hayaishi kila leo.

big up watu wa new york niambiyeni kiingilio kiasi gani nije please sijaona sehemu iliyosema kiingililo thank you

Anonymous said...

kama ni mtanzania na anaipenda nji yake basi afanye kama charity kwa ajii ya nchi yake siyo kila siku atake ku bookiwa na kulipwa kwa appearance zake kama ndo hivyo bora akae huko anapokaa na kufanya shughuli zake na sisi tunafaanya za kwetu kivyetu vyetu wa dc hawajatuzidi akili hata siku mmoja wameshazoea kukaa vibarazani vya vijiweni vya ughaibunin na kupiga domo kaya ndo maana kila leo wana vumbua vipati pati ndo kazi zao watu wa new york ni jembe kwenda mbele vitoto vya kidume vishoka siyo vishogaaaa.