Bais la Taifa Stars
James Karinge ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo wa kanda kupitia wakili wake Benjamin Mwakagamba wa Kampuni ya Uwakili ya BM wameyapinga maombi hayo ya TFF kwa madai kuwa hayana msingi pamoja na maelezo ya kuwa utekelezaji wa deni hilo umekamilika.
KAMPUNI ya Punchlines Tanzania Limited imewasilisha hati kinzani Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara ikipinga maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuomba ifanye mabadiliko ya kuliondoa basi lao lenye usajili namba T 581 CGR lililowekwa sokoni kuuzwa na kampuni hiyo kufidia deni la Sh56.8 milioni na badala yake liwe gari lenye usajili T 528 ASJ aina ya Coaster.
James Karinge ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo wa kanda kupitia wakili wake Benjamin Mwakagamba wa Kampuni ya Uwakili ya BM wameyapinga maombi hayo ya TFF kwa madai kuwa hayana msingi pamoja na maelezo ya kuwa utekelezaji wa deni hilo umekamilika.
Mwakagamba alihoji kwa nini TFF inataka kubadili dhamana kana deni limekamilika
“Maombi haya hayana msingi, yamegundulika na hayana uthibitisho wa nyaraka zinazohusu basi dogo lenye usajili T 528 ASJ aina ya Coaster,” alieleza Benjamini kwa niaba ya mteja wake.
TFF iliwasilisha maombi yao pamoja na hati ya kiapo iliyosainiwa na Katibu Mkuu ,Mwesigwa Selestine mahakamani Septemba 16, 2014 na Septemba 18, 2014 yakapangwa mbele ya Jaji Kassim Nyangalika.
TFF iliomba ifanye mabadiliko ya kuliondoa basi lao lenye usajili namba T 581 CGR lililowekwa sokoni kuuzwa na Kampuni ya Punchlines Tanzania Limited kwa ajili ya kufidia ya deni la Sh56.8 milioni na badala yake liuzwe gari lenye usajili T 528 ASJ aina ya Coaster.
Kwa mujibu wa maombi hayo yanayotarajiwa kusikilizwa Oktoba 7, 2014 na Jaji Nyangalika, TFF wanaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kulibadilisha basi lao lenye usajili namba T 581 CGR lililokamatwa na Kampuni ya Punchlines Tanzania Limited ili kufidia deni la Sh56.8 milioni na badala yake liwe gari lenye usajili T 528 ASJ Coaster.
TFF pia wanaiomba mahakama kuondoa hati ya kukamatwa kwa magari yake kwa maelezo kuwa Kampuni ya Punchlines Tanzania Limited imeshalipwa deni lake lote.
Pia, wanaiomba mahakama kutoa amri kuwa Kampuni ya Punchlines Tanzania Limited ilipe gharama za kesi na maombi hayo ambayo yamesajiliwa mahakamani hapo.
TFF inadaiwa zaidi ya Sh141 milioni na Kampuni ya Punchlines Tanzania Limited kutokana na kupewa huduma ya kusambaziwa tiketi kwa mkopo, fedha ambazo ziliongezeka na kufikia kiasi cha Sh159, 454,902.32. TFF ilifanikiwa kulipa Sh102.6 milioni kati ya Agosti 26 na 27, 2014 na bado wanadaiwa Sh56.8 milioni, hivyo wameliweka basi lao hilo sokoni.
Credit:Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment