Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu waserikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki. Mara baada tu yakuingia ukumbini.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula.
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani –Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na Serikali Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI
YA DUNIA NA IMF YAANZA MIKUTANO YA MWAKA
MJINI WASHINGTON DC - MAREKANI
Kila mwaka Bodi ya
Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana
kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi
zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake
hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC
kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi
mwanachama.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka
Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja
na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu
ambaye pia ni Gavana katika mikutano
hii.
Mikutano hii inatoa
nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la
Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za
mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya
kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza
kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi.
Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji
fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha.
Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na
mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira.
Hali ya hewa mjini
hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington
D.C
7/10/2014
No comments:
Post a Comment