ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 7, 2014

Chadema yavuna wanachama 130 wa CCM.

na Bryceson Mathias, Korogwe vijijini.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika mkutano wake uliofanyika Korogwe hivi karibuni, kimevuna wanachama 130 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), huku kikimtolea uvivu Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo, kikimtaka aacha ofisi avae nguo za CCM, kipambane nae kwenye majukwaa ya siasa.
Kilichomponza Gambo, ni Kauli aliyoitoa kwenye Mkutano wa hadhara wa Katibu wa CCM, Abdulahman Kinana, uliofanyika Mombo, ambapo alidai, aliwapa Chadema Kibali cha kufanya Mkutano Korogwe Ijumaa, Septemba 26, 2014, lakini anashangaa hawakufanya.

Akihutubia Mkutano wa Hadhara uliofanyika Septemba 27, katika Viwanja vya Sokonl Stand, Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga, Jonathan Bawaje, alimshambulia Gambo aache kuibeba CCM, la sivyo aiache Ukuu wa Wilaya avae Nguo za CCM, arudi jukwani kisiasa jukwani.

“Wananchi; Gambo si Polisi wa kutupa kibali cha Mkutano; isipokuwa anafanya Propaganda akiwa na lengo, na ndiyo maana anapita na timu vijijini akiwatisha wananchi kuwa asiyelipa Sh.30,000/- za Ujenzi wa Maabara kwa Kaya atachukulia hatua; Mpuuzeni ana lake!.

“Tunawashukuru watu wa Kwagunda ambao walikataa kuchangia Ujenzi wa Maabara na Maendeleo, hadi Gambo amsurubu, Mbunge wao, Stephen Ngonyani, kabla hajawasurubu wao, aliyeahidi wasilipe fedha kuwa atatoa Saruji Mifuko 100 na Bati 100”.alisema Bawaje.

Mbali ya Chadema kuishutumu CCM kuendesha Mafunzo ya Green Guard Bungu, ili wavuruge mikutano na kushusha Bendera zao zikiwemo Saba walizoiba, wamelaani Mtendaji, Bakari Layumba, Makorola, kuwatoza watu sh. 30,000/- za Maabara kwa Kaya, bila kuwapa risiti.

Aidha katika Kikao chake cha ndani cha Chadema Septemba 28, Chadema kilivuna Kadi 30 za CCM Makorola, baada ya kumwekea dhamana na kumtoa Polisi, Ringo Mjenga, aliyekamatwa akidaiwa Mchochezi, kwa kuhoji Mapato na Matumizi ikiwemo Idadi ya wanakijiji wanaolipa sh.30,000/-.

No comments: