ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 7, 2014

FIGISU FIGISU ZA VIONGOZI WA YANGA NA SIMBA WAKIWA MBIONI KUOMBA MADARAKA


Uwanja wa Simba Bunju aibu tupu
By MWANAHIBA RICHARD NA GIFT MACHA 

Mwanaspoti ambalo limekuwa likifuatilia eneo la uwanja huo tangu mwanzo, juzi Jumamosi lilifanya ziara kwenye uwanja huo ili kujionea maendeleo yake lakini hali iliyokutwa sio ya kuridhisha.
Katibu mkuu aliyeondoka madarakani Simba, Ezekiel Kambwaga aliukabidhi uongozi mpya wa klabu hiyo kiwanja hicho cha Simba kilichoko Bunju mwisho nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kikiwa kimefanyiwa usafi na kutengenezwa kwa eneo la uwanja wa mazoezi ambalo lilipandwa nyasi lakini kwa sasa hali imerejea kuwa mbaya kwani hakuna matunzo yoyote yanayofanyika kwenye uwanja huo ukiwemo umwagiliaji wa maji.

Mwanaspoti ambalo limekuwa likifuatilia eneo la uwanja huo tangu mwanzo, juzi Jumamosi lilifanya ziara kwenye uwanja huo ili kujionea maendeleo yake lakini hali iliyokutwa sio ya kuridhisha.

Hakuna Nyasi

Eneo hilo lilikuwa limepandwa nyasi za kisasa kutoka mkoani Mbeya ambazo zilipaswa kumwagiliwa maji ili zikue lakini kwa sasa zimetoweka zote na uwanja huo umejaa magugu pekee.

Uwanja huo ambao viongozi walijigamba kuwa wataanza kuutumia kwenye mzunguko wa pili wa Ligi haufai hata kwa matumizi ya mechi za mchangani ‘ndondo’ kutokana na kujaa magugu hayo marefu na mengine yenye miiba.

Nyasi za uwanja huo zilizokuwa zimepandwa zilipaswa kumwagiliwa ili zikue lakini utafiti mdogo uliofanywa na Mwanaspoti ulibaini kuwa eneo hilo halijamwagiliwa maji kwa muda mrefu sasa.

Licha ya uwepo wa magugu bado eneo hilo lilionekana kuwa kavu na jambo linaloashiria kuwa siku ya mwisho kumwagilia maji eneo hilo haikumbukwi.

Eneo hilo la uwanja limekabidhiwa kwa mlinzi ambaye analinda magoli yaliyowekwa nje ya kibanda chake cha mabati anachokitumia uwanjani hapo.

Kibanda hicho cha mlinzi kiwanjani hapo kinatia aibu kwani kinafanana na nyumba za waathirika wa mafuriko katika eneo la Jangwani, viongozi wa Simba wameshindwa hata kujenga kijumba kidogo cha kisasa ili kuendana na hadhi ya klabu hiyo.

Uongozi uliopita ulitumia zaidi ya Sh 100 milioni kumlipa mkandarasi huyo ambaye alifanya kazi yake ya awali na kazi iliyokubaki imebaki ni usimamizi tu kutoka kwa viongozi wa sasa ambao wameahidi ifikapo Aprili mwakani tayari watakuwa wamejenga hosteli kwa ajili ya wachezaji wao kwani utakuwa umeanza kutumika.

Jengo la Simba lameremeta

Baada ya uongozi wa Ismail Aden Rage kuondoka madarakani Simba, viongozi wapya wameamua kufanya kufuru ndani ya muda mfupi kwa kulikarabati jengo la ofisi la klabu hiyo kwa kiasi kikubwa.

Jengo hilo ambalo limekuwa likionekana kuwa chakavu kwa sasa limekaribia kuonekana kuwa la kisasa kutokana na ukarabati huo.

Mwanaspoti ilifanya ziara kwenye jengo hilo na kukuta mafundi wakiwa bize kupaka rangi na kurekebisha sehemu nyingine ndogondogo ambazo tayari zilianza kuleta mvuto.

Kazi ya kupaka rangi tayari inaonekana kukamilika kwa karibu asilimia zote kwa ndani huku ikibaki eneo la nje tu ambalo ndilo limebeba taswira ya eneo hilo.

Pia jengo la pili la klabu hiyo limeonekana kuwa safi na kuchangamka zaidi baada ya uongozi huo mpya kuingia.
Credit:Mwanaspoti

No comments: