HALMASHAURI
Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imemaliza kikao chake cha siku mbili
chini ya Mwenyekiti wa CCM Dkt. JAKAYA KIKWETE ambapo pamoja na mambo
mengine imepokea taarifa ya mchakato wa Katiba na kulipongeza bunge
hilo.
Aidha imeunga
mkono kwa asilimia mia moja Katiba hiyo pendekezi na kuwataka wananchi
waisome,kuitafakari na wakati ukifika wajitokeze kwa wingi na kupigia
kura ya ndio.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mjini Dodoma, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
ndugu NAPE NNAUYE amesema NEC wamelipongeza Bunge hilo kwa kazi nzuri
iliyofanya.
No comments:
Post a Comment