Sunday, October 26, 2014

HASHIM LUNDENGA AKANUSHA HABARI ZA SITTI MTEMVU aka MISS TANZANIA KUJIVUA TAJI.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga (kati pichani), amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani kushoto) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014).

Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru. “Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.

Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu. “Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo na. bado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.

Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.” ‪

8 comments:

Anonymous said...

The lack of integrity, leadership and ethics in this episode is amazing. The mother's arrogance, naivety, indecency and foolhardiness is similarly stunning! We are watching a train wreck approaching a cliff! It cannot go on for long! Why are they blind to this reality? Only in Tanzania!

Anonymous said...

not only in Tanzania mdau hapo juu ita all over the world sema wao wanaficha tu makucha yao,chunguza utakuja kuona mambo mengi tu nayo hawayapitishi sawa.chanzo cha ebola nini na kwa nini wanawadanganya wananchi wao na kwa nini wanajaribu kuwatenga walio toka Africa hao manasi.

that's not good/cool at all kila siku kuwailaumu nchi yetu kama ni mbaya hivyo mbona hao hao wanakwenda na kuchimba migodi na kuruka nayo huko kwao na kufaidi.

think outside of the box mkuu.

Anonymous said...

I think the best solution for Bi Sitti is to leave the Taji na kuendelea na maisha yake. She has a lot in life, she is beautiful, she has a degree and she speaks French. She has a family that's close to her. What else does she want? The situation can be managed in Tanzania, before she goes to Miss World. The moment this gets out of the CCM jurisdiction she is in deep trouble.
Sitti you can have a happy life without being Miss Tanzania, work hard on your studies and enjoy. Aren't you tired already? life is short dear, enjoy!

Anonymous said...

hili kweli linasikitisha na ni aibu. huyu dada, wazazi wake, pamoja na waandaaji wa mashindano haya wote wanahitaji msaada.

Anonymous said...

Very true! Only in Tanzania.

Anonymous said...

OK. Not only in Tanzania! Can't we be different? You want to think out of the box? Try this: Wengine wakiwa hawana maadili sio sababu nasi tusiwe nayo!

Anonymous said...

THEY SAY "IT IS NOT A LIE UNTIL YOU GET CAUGHT"

Anonymous said...

that right kama ccm they get caught all the time and the say its not me.
nikweli wasio na maadadili tuwacha na sisi tulionayo tusiyaache.

nchi yetu nzuri sana Tanzania yetu,wageni wanaithamini; wazawa tunaiponda,why?think outside the box.