Advertisements

Monday, October 20, 2014

Je nyama hii ndio chanzo cha Ebola?

Nyama ya wanyamapori ambayo huchomwa au kupikwa huwa haina athari sana mwilini 
Raia wengi wa Afrika Magharibi hula nyama ya wanyama wa msituni
Popo wanaokula Marunda wanaaminika kubeba virusi vya Ebola lakini huwa wahaonyeshi dalili za kuambukizwa virusi hivyo
Zaidi ya Popo 100,000 huliwa nchini Ghana kila mwaka

Nyama wa wanyama wa msituni ndio inaaminika kuwa chanzo cha mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa janga kwa mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi na kwa ulimwengu wote.

Familia ya Mwathiriwa wa kwanza wa Ugonjwa huo iliwinda Popo ambao huwa na virusi vya Ebola.

Lakini katika baadhi ya wanyama hawa huwa wamebeba magonjwa hatari.

Kama Popo huwa wamebeba virusi aina tofauti ambavyo ni hatari kwa mwili wa binadamu huku baadhi ya Popo wanaokula matunda wakiwa na virusi vya Ebola.

Kinyesi cha wanyama hao kilicho na virusi hivyo kinaweza kuwaathri wanyama wengine kama vile Nyani na Sokwe.

Kwa wanyama hao kama kwa binadamu virusi hivyo vinaweza kuwa hatari.

Lakini Popo wanaweza wasiathirike sana.

Kwa hivyo inakuwa rahisi kwao kubeba virusi hivyo bila ya kuathirika kwa vyovyote.

Je ulaji wa nyama ya wanyama wa msituni inaweza kuwa ndio chanzo cha janga la Ebola ambalo limekumba hasa kanda ya Afriak Magharibi?

Kitovu cha janga hilo kimesemekana kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili kutoka kijiji cha Gueckedou Kusini Mashariki mwa Guinea, eneo ambalo nyama Popo ambayo huwindwa na kuliwa mara kwa mara.

Mtoto huyo aliyesemekana kuitwa, Child Zero, alifariki tarehe sita Disemba mwaka 2013.

Hata hivyo haijulikani ambavyo virusi hivyo vinaathiri mwili wa binadamu, kulingana na Profesa Jonathan Ball,mtaalamu wa virusi katika chuo kikuu cha Nottingham.

Anasema inawezekana virusi hivyo hupitia kwa wanyama kama Nyani lakini ushahidi unaonyesha kuwa virusi hivyo pia vinaweza kupitia kwa Popo.

Hata hivyo anasema ni vigumu kwa virusi kutoka kwa mnyama hadi kwa binadamu.

Anasema mwanzo virusi vinaingia kwa seli za mwili ambapo vinazaana kwa kuugusana na damu mwilini.

Familia ya mtoto huyo,ilisema kuwa iliwinda aina mbili ya Popo ambayo huwa na virusi vya Ebola.

Nyama ya msituni inaweza kutoka kwa Nyani, Popo wanaokula matunda na wakati mwingine hata kutoka kwa Panya na Nyoka.

Kutoka katika maeneo mengine nyama hii huwa ni mlo muhimu kwa jamii lakini kwa wengine hula tu kama njia ya kufurahisha nafsi zao.

Nchini DRC watu hula milioni ya tani za nyama ya wanyama wa msituni kwa mujibu wa shirika la utafiti la (Centre of International Forestry Research,) kila mwaka.

Sio nchini DRC pekee ambako nyama ya wanyama wa msituni huliwa bali pia nchini Ghana.

Lakini cha kushangaza ni kwamba hapajakuwa na hata kisa kimoja cha maambukizi ya Ebola nchini Ghana

BBC

9 comments:

Anonymous said...

kuna watu wanakula popo bawa hawa, ebwaana eeh, balaa mkuu.waafrica sisi mwishoooo

Anonymous said...

Unajua huu ugonjwa ni porojo tu...swali kama kweli upo huko west africa kwanini wapeleke wanajeshi wa kutosha wenye zana za kivita nzito badala ya kupeleka madaktari wengi? Pia congo ilikuwepo ebola then ikaondoka....je sababu iliyofanya ebola izaliwe congo na pia ife huko huko congo ni ipi? God bless Africa, God save Africa...

Anonymous said...

Isijekuwa kama Dengue, ambayo sasa sijui iko wapi jamani baada ya Watu kulalama kuwa ulikuwa mpango wa Serikali.

Ziko wapi ripoti za huu ugonjwa wa ebola au ni kisa kasema mzungu nasi tunakimbilia tu.

Ila, as long as tutaendelea kuwategemea wao kwa ukombozi wa matatizo yetu daima tutaangamizwa. Mbona wa China wahindi hili janga halijawapiga kama sisi?

Ila nilichokuja gundua ni kwamba kwa sisi waafrica hata kama wote wakiambiwa na wakijua hatuna uwezo wa kufanya chochote sababu hatuna nguvu ya umoja. Ni ajabu sana lakini mzungu ana uwezo mkubwa sana wakutufanya tulumbane wenyewe kwa wenyewe na tushindwe kuaminiana wenyewe kwa wenyewe lakini tumwamini mzungu.

mungu peke ndo mkombozi wetu.

Mimi sijakubali niliyoyasoma katika hii habari, nyie chomeni!

Anonymous said...

danganya toto hizi ebola ina spreak wakati ukipigwa sindano zake za kuuzuia huu ugonjwa. kama unabisha kwa nini mliberia amekufaa texas na unajua kwamba Nigeria wameshapata dawa za hizi ebola.unajua serikali ya Liberia na Nigeria imewafukuza Red cross na chanjo zao kwa sababu wamewashtukizia.

chunguzeni mtajua chanzo cha huu ugonjwa na si eti hawa wanyama na nyama hizi .chunguzeni kwa nini wanakwenda Nigeria na Liberia.

msiwe wavivu ndugu zangu kuchunguza vyanzo vya mambo yaanavyopikwa kwenye chungu.


Anonymous said...

hakuna msaada wa Mmarekani au mgeni mwingine yeyote wenye lengo kamili la kutuokoa. tunahitaji knowledge. Tunahitaji kufundishwa kuvua samaki ili tuweze kuvua wenyewe na sio kutuletea samaki tule(funds).

tujiulize ugonjwa wa dengue umepotelea wapi hivi sasa hapa nyumbani Tanzania,na vyandaruwa vimepigwa dawa na dawa hii inadumu kwa miaka 5 hata ukikifua hicho chandarua dawa hapotei nguvu yake pale pale na wanakilalia mama waja wazito na watoto wenye chini ya miaka 5. tujiulize malaria mbona mpaka hii leo tunayo na haijatokomea.kwanini wasitupe knowledge yakujifunza kuwaangamiza hawa mbuu.

mungu isaidiye na ibariki Africa na watu wake amen.

Anonymous said...

may God be with us all.
Amen

Anonymous said...

Magonjwa yote ya kutisha hutengenezwa na yanatiba. Ni bahati mbaya lengo la watengenezaji wa huu ugonjwa ni kuwaangamiza watu weusi duniani.

ukienda america na ulaya mpaka chanjo ya malaria ipo ilhali hapa bongo hailetwi wakati ndipo kuna malaria mno. Tena kama europe au nchi zozote za weupe (majority) UKIMWI is not an issue ila kwa black majorities ni issue.

Anonymous said...

Halafu utasikia Mwafrika mwenzako anakwambia ni kwa sababu sisi waafrika tunawaza ngono tu mda wote na hatuvai condom! Unaweza mrukia kichwa aisee.
umesoma kuhusu immunity ya ukimwi walionao wazungu kutokana na mutation ya protein CCR5?
Je ulishawahi kusikia Plague, au the black death iliyokumba ulaya karne ya 14?

Unajua inasemekana ilikua ni kirusi kama EBOLA!! Sasa imeanzeje ghafla WA?

Was Ebola Behind the Black Death? - ABC News

Anonymous said...

Sehemu nyingi za Africa wanatabia mbaya ya kutaka kula vituvisivyo wezekana kama Kima, Panya na vinginevyo…



1.Mtu unakula panya na unajua kabisa kuna watuwanazikwa kiholelahola bila majeneza wala kujengea kabuli, hao panya wenyewemnaokula mnawatoa kwenye mashimo je unauhakika gani kwamba unachokula hakitakuzulu?

2.Kima yeye ni mnyama mwenye vijidudu kibaomwilini mwake nabado watu wanamla, unategemea nini?



Mimi naona serikali za Africa zenye wananchi wanaokula vitu vya ajabu ajabu watume watu wao huko China wakajifunze jinsi ya kutoa sumu kwenye hivyo vitoweo kusudi wasalimike la sivyo wataendelea kutupa matatizo huko mbeleni, waafrika tunatakiwa tuanze kumtafuta mchawi ndani ya nyumba zetu kabla ya kuanza uzushi