Advertisements

Wednesday, May 1, 2024

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapungia mkono Wafanyakazi mbalimbali waliojitokeza katika Sherehe za Mei Mosi wakati akiwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01 Mei 2024. Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01 Mei 2024. Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapungia mkono Wafanyakazi wakati wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.
Wafanyakazi kutoka Wizara,Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa ujumbe kuhusiana na masuala mbalimbali ya Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.

No comments: