ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 1, 2024

JIEPUSHENI NA “MAFATAKI”

Na Issa Mwadangala

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bupigu iliyopo Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wametakiwa kujiepusha na vishawishi vya mafataki wanaotaka kukatisha ndoto ya safari ya masomo yao.

Hayo yalisemwa Aprili 30, 2024 na Kaimu Kamanda Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyera alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara ya mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Kamanda Hyera alisema “Jukumu la ulinzi wa wanafunzi na watoto ni letu sote hivyo basi kila mmoja anapaswa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupinga ukatili ili ujumbe ufike kwa wepesi kwa jamii jambo ambalo litapelekea kupunguza ukatili katika mkoa huo”.

Kamanda Hyera alitoa wito kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili na uhalifu kuacha mara moja na endapo mwanafunzi au mtoto aonapo viashiria au afanyiwapo vitendo vya ukatili kama vipigo, ubakaji, ulawiti anatakiwa atoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments: