ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 6, 2014

Kutuma Mchango Wako

Ndugu Mwana Mfuko,

Tunakushukuru sana kwa kuendelea kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Mfuko wetu wa Jumuiya ya Watanzania hapa Ohio. Katika hatua ya kufanya maboresho ya utaratibu wa kuendesha Mfuko, tungependa msaada wako katika utaratibu wa kuweka mchango wako benki.

Unapoenda kufanya deposit benki, tungeomba uweke jina lako na sababu ya mchango wako katika deposit slip. Mfano "Metty - Msiba wa Deo Mwalujuwa" au "Metty - Uanachama". Hiyo itasaidia sana kuweka rekodi zetu sawa na kwa urahisi kwa sababu benki wanatupa taswira (image) ya deposit slip. 

Kama una swali lolote kuhusu huu utaratibu, au kama una pendekezo lolote juu ya namna ya kurahisisha huu utaratibu, tafadhali wasiliana na Uongozi wa Mfuko. 

Tunatanguliza shukurani zetu.

Uongozi wa Mfuko

No comments: