Advertisements

Friday, October 17, 2014

MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA PSPF NI MKOMBOZI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adfam Mayingu, (Wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, (Wapili kushoto) na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko huo, .Mwanjaa Seme, wakiwafafanulia huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko, baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja ya mameneja rasilimali watu kutoka wakala za serikali, mwishoni mwa warsha hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo
Mgeni rasmi Peter Ilomo, (Suti Nyeusi katikati waliokaa), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adma Mayingu, (Watatu kulia), na baadhi ya viongozi wa juu wa Mfuko huo, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Meneja wa Mpango wa Uanachama wa Hiari, Mwanjaa Seme, (Kushoto), akiendelea kutoa somo kwa wadau
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizunfumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa maafisa rasilimali watu kutoka wakala za serikali iliyofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Alhamis
Meneja Masoko, na Mawasiliano wa PSPF, Constatina Martin, akitoa muongozo wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa
Mwnasemina akilonga
Maafisa waandamizi na wafanyakazi wengine wa PSPF, waliofanikisha semina hiyo, wakiwa katika picha ya ukumbusho
Katibu Mkuu Ilomo akitoa hotuba yake
Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo, (Kulia) na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Gabriel Silayo, wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano
Silayo akiwasilisha mada

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu Bw. Peter Ilomo amewashauri watanzania kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ili kujiongezea kipato na hatimaye kuishi ya staha.
Bw. Ilomo alisema hayo Mjini Bagamoyo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya Maafisa Rasilimali Watu kutoka wakala mbalimbali za Serikali
Kutokana na mabadiliko kwenye sekta ya hifadhi ya jamii, PSPF ilianzisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari maarufu kama PSS ili kuweza kuwahudumia Watanzania wote ambao wanahitaji huduma za hifadhi ya jamii ambao walikosa fursa hiyo huko nyuma.
“Mpango huu ni mkombozi kwani unazidi kukuongezea kipato na kukufanya uishi maisha yenye staha sasa na hata wakati wa ustaafu wako. Mpango huu pia unatoa ruksa kwa mtu asiye raia wa Tanzania lakini anafanyakazi hapa nchini kihalali kuwa mwanachama” alisema Bw. Ilomo.
Akizungumzia juu ya ujio ya kanuni moja ya ukokotoaji wa mafao, Bw. Ilomo alisema, “Kuwepo kwa kanuni moja ya ukokotoaji mafao ni changamoto kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kwa kuwa kigezo kikubwa cha kuvutia wanachama kitakuwa ni ubora katika huduma na mafao ya muda mfupi. Hivyo, nawaagiza watendaji wote wa PSPF kuhakikisha mnatumia vyema fursa hii kutoa elimu sahihi kwa watendaji hawa muhimu katika utumishi wa umma hapa nchini”.
Kutokana na Wizara ya Kazi na Ajira kutangaza kuwa Mifuko yote ya Hifadhi ya itakuwa ikitoa mafao yanayolingana, alisema wanachama wa PSPF waliokuwepo hadi tarehe 30/6/2014 watalipwa kwa utaratibu wa zamani na wote walioajiriwa kuanzia Julai 1, 2014 watalipwa mafao yao kwa mujibu wa kanuni mpya.
Katibu Mkuu huyo kutoka ofisi ya Rais aliipongeza PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuongeza, “ Semina hizi ni muhimu kwani zinatoa fursa ya kuonana na wadau na kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwa manufaa ya Mfuko na wanachama wake”.
Awali akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliwahakikishia washiriki wote wa semina hiyo kwamba PSPF itahakikisha inafikia dira yeke ambayo ni kuwa mtoa huduma bora wa hifadhi ya jamii nchini, na kufanyakazi kwa mujibu wa dhima ya Mfuko ambayo ni kutoa huduma zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wake kwa kutumia watumishi wenye ari ya kazi na teknolojia inayofaa.
Katika kuhakikisha inafikia dira yake na kuishi dhima yake, Bw. Mayingu aliahidi kwamba PSPF itaendelea kutekeleza majukumu yetu ya utendaji wa kila siku ikiongozwa na uwajibikaji, wajibu, muitikio, nidhamu, juhudi, uwazi na unyenyekevu kwa wote.

No comments: