Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la lillojulikana kwa jina la Tanzania Movie Talent (TMT) Mwanaafa Mwinzago, msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam baada ya kujinyakulia milioni 50, anasema kuwa anafanya mipango ya kusoma Dar es Salaam na si Mtwara tena.
“Nilirudi Mtwara kwa ajili ya kufanya mtihani wangu wa darasa la saba, na nimerudi Dar tena kwa ajili ya kurekodi filamu ya TMT Movie, siwezi tena kurudi Mtwara nitasoma hapahapa tu,”anasema Mwanaafa.
No comments:
Post a Comment