Mwanasheria na mdau mkubwa soka nchini,Damas Ndumbaro.
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limemfungia miaka saba mwanasheria na mdau mkubwa soka nchini Damas Ndumbaro kujihusisha na soka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa madai kuwa amekiuka Kanuni za Ligi za shirikisho hilo.
Akisoma hukumu hiyo kwenye ofisi za Makao Makuu ya TFF zilizopo Posta jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo, Jerome Msemwa, alisema kamati imemtia hatiani mwanasheria huyo kutokana na kauli alizozitoa hivi karibuni kuhusu maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukata fedha za udhamini wa klabu na mapato ya milangoni.
Ndumbaro, akiwa wakili wa klabu za Ligi Kuu, alikutana na waandishi wa habari jijini mwanzoni mwa mwezi na kueleza kuwa wateja wake (klabu) wanapinga uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF kukata asilimia tano ya fedha za udhamini na Sh. 500 ya kila tiketi inayokatwa na shabiki kuingia uwanjani.
Ndumbaro pia alidai kuwa Kanuni za Ligi zilizopitishwa kutumika kwa ajili msimu huu, hususan kuhusu makato ya fedha za milangoni si sahihi kwa vile zimerekebishwa na Kamati ya Mashindano ya TFF badala ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo.
Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa dakika 25 kuanzia saa 8:25 hadi saa 8:50 alasiri jana, Msemwa alisema Ndumbaro kama mjumbe wa Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba, hakupaswa kutoa kauli hizo dhidi ya TFF kwa vile ni mwanachama hai wa shirikisho hilo.
"Ndumbaro ambaye ni mwanasheria, ni mwanachama wa TFF kwa sababu ni mjumbe wa TPLB na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba, hivyo ana 'conflict of interest' (maslahi binafsi) na TFF. Kama kiongozi wa TFF amevujisha siri za shirikisho kwa manufaa ya wateja wake," alisema Msemwa.
Alisema amepatikana na hatia ya kutoa tuhuma zisizo sahihi, kupotosha umma kuhusu Kanuni mpya za Ligi na kuzuia utekelezaji wa maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF ilhali akijua yanaweza kutenguliwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama wa shirikisho pekee.
Wakili huyo alisema kamati imeridhika na ushahidi wa upande mmoja uliotolewa na Sekretarieti ya TFF kupitia kwa Mkurugenzi wa Wanachama wa shirikisho hilo, Eliud Mvella, hivyo kumfungia Ndumbaro kujihusha na masula yote ya soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho.
"Kwa kuzingatia Ibara ya 41(6) cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014, kamati inamfungia Dk. Damas Daniel Ndumbaro kujihusha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 12," alisema.
"Pia kwa kuzingatia Ibara 41(16) cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014, kamati inamfungia Dk. Damas Daniel Ndumbaro kujihusisha na shughuli za soka ndani na nje ya nchi kwa miaka saba. Hukumu hii imetolewa leo (jana) Oktoba 13, 2014," alisema zaidi wakili huyo huku akifafanua kuwa mlalamikiwa atatumikia kifungo cha miaka saba kwa kuwa kifungo cha miezi 12 kinamezwa na kifungo kikubwa.
KESI YASIKILIZWA SIKU MBILI
Akieleza namna kesi hiyo ilivyoendeshwa kabla ya kutoa hukumu hiyo, Msemwa alisema wamesikiliza kesi hiyo kwa siku mbili; Jumamosi na Jumapili na hukumu ilitolewa bila uwapo wa mlalamikiwa.
Alisema baada ya kupelekewa malalamiko ya Sekretarieti ya TFF dhidi ya Ndumbaro, walimpelekea barua mlalamikiwa na kumtaka kufika kwenye kikao Oktoba 10. Alisema Ndumbaro hakufika mbele ya kamati hiyo lakini walipata taarifa za kutofika kwake kutoka kwa wakili wake, Nestory Peter.
"Kwa kuwa Ndumbaro hakufika mbele ya kamati, tuliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, mwaka huu kujadili kama tunaweza kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja ama la. Kwa kuwa Ndumbaro hakuleta ushahidi wowote kueleza mahali alipo, kamati iliamua kusikiliza kesi ya upande mmoja na kutoa hukumu," alisema.
Akielezea ushahidi wa TFF uliowasilishwa na Mvella mbele ya kamati, Msemwa alidai kuwa Ndumbaro alikiuka Kanuni za Nidhamu na Kanuni za Ligi za TFF kwa kuzisemea klabu, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuituhumu TFF kuziibia klabu, serikali na CCM kupitia makato ya milangoni huku akitishia kulishtaki shirikisho Fifa.
Aidha, Msemwa alisema TFF walidai Ndumbaro kama mwanachama wa shirikisho, amekiuka Kanuni za Ligi toleo la 2014 kwa kuwataka wadhamini wakuu wa Ligi Kuu, Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Azam Media waliyonunua matangazo ya televisheni ya ligi hiyo kujitoa.
Alisema Mvella aliwasilisha ushahidi wa magazeti na sauti za redio likiwamo gazeti la NIPASHE la Oktoba 4, mwaka huu lililotumika kama ushahidi Na. 4 likinukuu kauli za Ndumbaro dhidi ya TFF.
Msemwa pia alisema mlalamikaji aliwasilisha barua za klabu za Coastal Union ya Tanga na Stand United ya Shinyanga zilizotumwa TFF zikikana kumtuma Ndumbaro kutoa tamko hilo.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Coastal, Steve Mguto alikuwa miongoni mwa wawakilishi wa klabu kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam wakati Ndumbaro akitoa tamko hilo dhidi ya TFF.
Alipoulizwa kwa nini kamati yake haikumchukulia hatua za kinidhamu Ndumbaro alipoingilia usajili wa Emmanuel Okwi kwenda Simba siku chache kabla ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akimtetea Okwi ilhali alikuwa na maslahi binafsi na TFF, Msemwa alisema:
"Kama kuna makosa ya kisheria yalifanyika huko nyuma, yanawahusu walioamua. Kesi hii nimeisimamia mimi, hivyo nimeamua kulingana na ufahamu wangu wa sheria. Ndumbaro ana 'conflict of interest' na TFF. Huo ndiyo msimamo wangu katika hilo."
Kadhalika NIPASHE lilipotaka kujua kwanini kesi hiyo imeamuliwa haraka tofauti na nyingine ambazo huchukua muda mrefu, alisema wanafanya hivyo ili kutochelewesha maendeleo ya soka.
Ndumbaro anakuwa mtu wa kwanza kufukuzwa uanachama wa TFF tangu Kamati mpya ya Utendaji ya shirikisho hilo chini ya Rais Jamal Malinzi iingie madarakani usiku wa kuamkia Oktoba 28, mwaka jana.
Gazeti hili lilipomtafuta Ndumbaro jana kwa simu ambaye yupo nchini Marekani kwa shughuli zake binafsi ili kujua mapokeo ya hukumu hiyo, simu yake iliita bila majibu na lilipomtumia ujumbe mfupi (sms) haukujibiwa. Juhudi za kupata msimamo wake bado zinaendelea

.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake