Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema hawezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu.
Nyalandu amesema kuwa wadhifa wa kuongoza nchi ni mkubwa mno, ambao mtu hawezi kujichukulia uamuzi wa kuiomba nafasi hiyo isipokuwa mpaka atumwe na watu, huku akisema kuwa ingawa hana mpango wa kugombea urais, lakini hata yeye akitumwa anaweza kugombea.
Nyalandu aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wake na wandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, jijini Mbeya.
Alisema kuwa ili mtu awanie urais, ni vizuri kwanza akatumwa na watu kwa kuwa kazi hiyo ni kazi ya Mungu, inayohitaji moyo mkunjufu na mpana katika kuutumikia umma.
“Ninachosema, zamani, nasisitiza, kikao kilikaa, kikasema tumtengeneze mtu kwa mfano wetu, lakini kikao kingine pia kilikaa, kikasema tumtume nani, kwa maneno mengine niseme, kuna hizi kazi lazima kikao kikae, lazima kikao kikutume, mtu anayetafuta urais kwa sababu zake binafsi atakuwa tu haelewi kinachotakiwa katika hiyo kazi, ni kazi ya Mungu, lazima watu wakutume, kwa hiyo mimi ni nani kuanza kujitangazia kazi, kitu ambacho matakwa ya hiyo kazi ni kazi ya watu,” alisema Nyalandu.
Alisema kuwa kazi hiyo ni uwakilishi mkubwa kwa umma wote wa Watanzania, hivyo ni lazima kwanza watu wamtume ndipo atakapofikia maamuzi ya kugombea nafasi hiyo.
Hata hivyo, alisema kwa watu wote waliokwisha tangaza nia ya kugombea, wafanye hivyo kwa nia njema na kwa moyo mkunjufu na kamwe wasiende katika kupigana vita.
“Mimi nina matumaini kwamba kwa watu wote wenye nia ya kugombea, wafanye hivyo kwa moyo uliokunjuka, kwa moyo mkubwa, wasiende katika kupigana vita sababu haisaidii, kila mtu aanze kutafakari ataifanyia nini nchi yetu,” alisema Nyalandu.
Alisema kwa sasa angependa kuanza kusikia mijadala juu ya Tanzania ijayo baada ya Rais Kikwete kuifikisha nchi hapa alipoifikisha, wale wanaokuja wana maono gani juu ya nchi hii.
Akizungumzia juu ya tuhuma zilizotolewa na viongozi wenzake hususan Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema kuwa tuhuma hizo siyo za kweli na kwamba ulimi wa Waziri Lukuvi uliteleza katika hilo.
Alisema kuwa suala la mgogoro uliopo kwenye Jimbo la Lukuvi linatokana na uongozi wa Halmashauri hususan Baraza la Madiwani ambalo Lukuvi ni mjumbe kwa mujibu wa sheria kumleta mwekezaji ambaye amesababisha mgogoro unaolalamikiwa na wananchi.
Alisema kuwa mgogoro huo pamoja na kusababishwa na halmashauri yenyewe, umefikishwa kwenye ofisi yake na Serikali Kuu kwa ujumla kushindwa kuingilia kati kutokana na kuheshimu misingi ya utawala bora.
Alisema kuwa tayari amekwishatoa maelekezo kwa wahusika kuwa kama watahitaji ofisi yake iingilie kati suala hilo, ni lazima kwanza liondolewe mahakamani.
Kuhusu tuhuma za kuandikiwa barua tatu bila kuzijibu, Waziri Nyalandu alisema kuwa hajawahi kuona barua hata moja, huku akidai kuwa barua zinapopelekwa wizarani zinapitia kwa watu wengi kama vile masijala, kwa makatibu wake kabla ya kumfikia, hivyo hana uhakika kama kweli barua hizo ziliandikwa.
Waziri Nyalandu alisema kuwa kwa kiwango kikubwa vita anayokabiliana nayo wizarani inatokana na uamuzi wake wa kudhibiti uwindaji wa tembo kwa zaidi ya asilimia 50, hali ambayo sasa inaonekana kuwakera baadhi ya watu wenye maslahi na biashara hiyo.
Hata hivyo, alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika kusimamia rasilimali za Taifa kama ambavyo ameapa ili ziwanufaishe Watazania wa kizazi cha leo na kijacho.
“Rais Kikwete aliponiteua kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, hakuwa amekosea, inawezekana ni maono aliyoyapata kutoka kwa Mungu, hivyo basi siwezi kuogopa vitisho na maneno ya watu wanaotaka tu kufanikisha maslahi yao, nitaendelea kupambana kuhakikisha nazilinda, nazitunza na kuzilea rasilimali za Watanzania,” alisema Nyalandu.
Kuhusu madai kuwa huwa anakwenda nje ya nchi mara kwa mara na kwamba safari zake ni za kuisababishia serikali matumizi makubwa, alisema amekuwa akisafiri kwa shughuli maalum za serikali kwa lengo la kutangaza utalii pamoja na shughuli zenye maslahi kwa Taifa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake